Mungu anachukia kuachana (Malaki 2:16)

Mungu anachukia kuachana (Malaki 2:16)

(Masomo maalumu kwa wanandoa)


Kama unafikiria kuachana na huyo ulifunga naye ndoa ni jambo la busara,  basi fahamu kuwa unafanya jambo linalomchukiza BWANA MUNGU. Kwanini???.. ni kwasababu Mungu anachukia kuachana.

Malaki 2:16 “Maana mimi NAKUCHUKIA KUACHANA, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana”

Utauliza vipi kwa sababu ile ya Uasherati iliyotajwa katika Mathayo 5:32.

Mathayo 5:32 “lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini”.

Ni kweli Uasherati ndio sababu pekee ya uhalali wa ndoa kuvunjika, lakini bado biblia haijatoa amri au sharti kuwa pale uasherati unapotokea basi ndoa hiyo ivunjike..(kwamba haipaswi kuendelea) inapaswa ivunjwe!.. La! Biblia haitufundishi hivyo hata kidogo…badala yake biblia inatufundisha kusamehe!..

Bwana wetu YESU KRISTO alikuwa na sababu zote za kutotusamehe, lakini alitusamehe hivyo hivyo, vipi mimi na wewe!, tusipokuwa watu wa kusamehe tutawezaje kumpendeza Mungu au sisi wenyewe kusamehewa?

Hivyo suala la ndoa ni kusameheana na kuvumiliana kwa mambo mengi.. Sisemi kuwa uasherati uvumiliwe au upaliliwe ndani ya ndoa, la!.. bali pale mmoja anapoonekana kuvutwa na ibilisi ni wajibu wa mwingine kumrudisha kwenye mstari kwa kumvumilia na kumwombea pamoja na kumtengeneza kwa neno la Mungu mpaka atakaporejea katika mstari sahihi wa Imani.

Usimwache Mume/mke kwasababu ya zinaa, (Ni kweli ni jambo linaloumiza lakini jifunze kuvumilia na kusamehe na kutafuta namba ya kutengeneza)…itakufaidia nini kumwacha huyo na kwenda kuanza familia nyingine na huku tayari mna watoto?..

> Usimwache Mume/mke kwasababu ya magomvi ya hapa na pale, itengeneze nyumba yako kwa maombi na mafunzo ya Neno la Mungu.

> Usimwache Mume/mke kwasababu ya hali ya Uchumi.. tafuta namna ya kuyatengeneza na si kukimbia.

> Usimwache Mume/mke kwasababu ya ndugu zako au ndugu zake, marafiki zako au marafiki zake.

> Usimwache Mume/mke kwasababu ya Uzee au magonjwa au madhaifu aliyonayo.

Na kumbuka: Mume na Mke wanaozungumziwa hapa ni wale waliohalalishwa na Neno la Mungu, (maana yake waliofunga ndoa) na si wale wanaoishi kihuni (wamechukuana na kuishi kwenye chumba/nyumba, na hata wengine wamezaa watoto)..hao si wanandoa bali ni wahuni..Hao haya maandiko haya na mashauri haya hayawahusu kabisa.. badala yake wanapaswa waachane mara moja na watubu na kila mmoja akae kivyake!!!!, kwasababu wanafanya Uasherati.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako.

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

Usimwache mwanamke mchawi kuishi! Biblia ilimaanisha nini?

Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments