Wakrete ni watu gani na walikuwaje  waongo? (Tito 1:12)

Wakrete ni watu gani na walikuwaje  waongo? (Tito 1:12)

Swali: Biblia inasema wakrete walikuwa ni waongo na walishuhudiwa na nabii wao, je walikuwaje waongo  (walidanganya nini), na huyo nabii wao alikuwa nani?


Jibu: Wakrete ni jamii ya watu waliokuwa wanaishi mahali paitwapo “Krete” na Krete ni kisiwa kilichokuwepo katika nchi ya Ugiriki.

Sasa Mtume Paulo alimwandikia Tito waraka huu kumpa maagizo na maelekezo machache kuhusu kanisa na viongozi (katika uteuzi).. Kwa urefu kuhusiana na kitabu hiki cha Tito na maaelekezo Paulo aliyompa Tito kwa uongozo wa Roho Mtakatifu fungua hapa >>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.

Lakini kwa ufupi ni kwamba tabia mojawapo waliyokuwanayo watu wa Krete, ni UONGO, Walikuwa wanasifa ya kusema Uongo katika viwango vikubwa, kiasi kwamba mpaka mtu wa kwao, ambaye ni nabii wao wenyewe aliandika kuhusiana na tabia hiyo waliyonayo waKrete ya Uongo, pamoja na ulafi na uvivu.

Biblia haijamtaja huyo Nabii ni nani, na wala haijaandika kuhusu huo waraka, lakini hapa tunaona Mtume Paulo ana unukuu…”

Tito 1:12 “..MTU WA KWAO, NABII WAO WENYEWE, AMESEMA, WAKRETE NI WAONGO SIKU ZOTE, HAYAWANI WABAYA, WALAFI WAVIVU

Sasa tukirudi katika historia, alikuwepo mwana filosofia wa KRETE aliyeitwa “EPIMEDINES”.. Huyu alikuwa ni Nabii wa mungu wa kigiriki aliyeitwa “zeu”..ambaye anatajwa katika Matendo 14:12-13.

Huyu Epimedines pamojana na kuwa alikuwa ni nabii wa mungu huyo wa kigiriki, lakini pia alikuwa ni mwandika mashairi. Moja ya shairi lake aliloliandika (ambalo aliliandika kwa kumtukuza huyo mungu wao wa kigiriki aliyeitwa zeu) lilikuwa linasema hivi..

…“Walikutengenezea kaburi, takatifu, uliye juu (zeu), Wakrete, waongo siku zote, wanyama wabaya, wavivu wa tumbo. Lakini wewe hukufa: unaishi na unakaa milele. Kwa maana ndani yako tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu”…

Ni shari la kumtukuza mungu wao (zeu), lakini lilikuwa maarufu Krete kote kwani huyu Epimedines aliaminika na  wakrete wote kuwa ni nabii. Na Paulo kwasababu ni msomaji, aliujua huu ushairi, na hivyo katika kusisitiza dhambi ya wakrete ya Uongo kuwa ni kweli, ndio ananukuu hayo maneno ya nabii wao aliyewashuhudia kuwa ni waongo.

Lengo la Mtume Paulo si kumthibitisha nabii wao huyo La!.. bali kuthibitisha Uongo wa wakrete ambao watu wote wanauona hata walio wa Imani ya mbali… Hivyo ndio anamwonya Tito aukemee huo!.

Tunachoweza kujifunza ni kuwa UONGO ni mbaya, kwani biblia inashuhudia kuwa ibilisi ndiye baba wa Uongo, hivyo wote wadanganyi wote ni watoto wa ibilisi.

Yohana 8:44 “ Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo”.

Bwana atusaidie tushinde dhambi.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WANNE WALIO WAONGO.

Mzushi ni nani kibiblia? (Tito 3:10).

UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.

Mungu anachukia kuachana (Malaki 2:16)

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments