Masomo maalumu kwa wahubiri.
Isaya 29:16 “NINYI MNAPINDUA MAMBO; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?”
Kama Mtumishi/Mhubiri jihadhari na MAPINDUZI yasiyo na msingi!.
USIIPINDUE INJILI YA KRISTO KWASABABU YA TAMAA YA FEDHA.
Unapoanza kuwadanganya watu wa wenye nia ya kumtafuta Mungu, ili tu upate fedha kutoka kwao!.. unapoanza kuwatumainisha watu wa Mungu mambo ya uongo ili tu uwatoe fedha!.. Hiyo ni ishara mbaya na hatari kubwa sana kwako!. Bwana ataenda kukupindua nawe pia!.
Tito 1:11 “Hao WANAPINDUA watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu”.
Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kufanya biashara katika nyumba ya Mungu (ambayo ni wewe mwili wako sawasawa na 1Wakorintho 3:16) kwa kuanza kufanya uasherati na uzinzi na ukahaba fahamu kuwa Bwana naye atakupindua (Soma 1Wakoritho 6:19).
Ukilipindua Neno la Mungu kwa kuiharibu nyumba yake (kama jengo) kwa kuanza kufanya biashara ndani yake na kufanya yasiyofaa Bwana YESU atazipindua meza zako (soma Mathayo 21:12)
Ukilipindua Neno la Mungu juu ya utakatifu wa mwilini na rohoni (sawasawa na 1Wathesalonike 5:23) na kuanza kufundisha/ kuhubiri kuwa Mungu haangalii mwili bali anaangalia roho tu peke yake ni kupindua maandiko ambako matokeo yake ni Mungu kuyapindua maneno yako na wewe kwa ujumla.
Mithali 22: 12 “Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali HUYAPINDUA MANENO YA MTU HAINI”
Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kuhubiri kuwa YESU KRISTO bado sana arudi, au kwamba hakuna mwisho wa dunia, huko ni kupindua mambo ambako matokeo yake ni mabaya kama ya Fileto na Himenayo.
2Timotheo 2:17 “na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata KUIPINDUA imani ya watu kadha wa kadha”.
Kama Mhubiri Ni heri KUPINDUA ulimwengu kwa mambo ya kweli ya INJILI kama walivyofanya Mitume wa kanisa la kwanza kuliko kuigeuza/kuipindua injili kwa faida zetu wenyewe.
Matendo 17:6 “na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa WALIOUPINDUA ULIMWENGU WAMEFIKA huku nako”
Siku ya Mapinduzi makuu inakuja, ambapo Bwana ataipindua dunia yote kama alivyoipindua miji ya Sodoma na Gomora (soma Kumbukumbu 29:23) na kipindi cha gharika ya Nuhu (Soma Ayubu 12:15).
Ezekieli 21:27 “NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa”
Hegai 2:22 “nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake”.
Usipindue Mambo yaliyonyooka, bali pindua yale yaliyopotoka.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
About the author