USIPENDE USINGIZI USIJE UKAWA  MASKINI.

USIPENDE USINGIZI USIJE UKAWA  MASKINI.

Mithali 20:13 “Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula”.

Usingizi unaozidi unachelewesha utekelezaji wa majukumu ya muhimu. Kwamfano Mwanafunzi anayelala kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa shule, vilevile mfanyakazi alalaye kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa kazini, mfanya biashara anayealala kupita kiasi ni lazima atachelewa kuanza biashara  yake.

Upo usemi usemao “biashara ni asubuhi” maana yake kwa mtu anayefanya biashara labda ya kuuza duka, asubuhi ndio wakati wa kufungua bishara maana watu wengi wanawahi kutafuta bidhaa asubuhi Zaidi ya mchana, hivyo alalapo sana hatapata zile faida za asubuhi, na hivyo yupo hatarini kufilisika.

Atapanga kweli kuwahi kuamka mapema kesho, lakini ifikapo asubuhi kitanda kinakuwa na nguvu kuliko maamuzi yake, atajiongezea muda wa kulala, na mwisho wa siku atashtukia kumeshapambazuka na jua linawaka..na hayo ni matokeo ya kusema “bado kulala kidogo”.

Mithali 6: 9 “Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?

10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!

11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.

Sasa biblia ni kitabu kilichojaa hekima ya kumwongoza mtu hata katika maisha ya kawaida Zaidi yay ale ya rohoni…. ni kitabu kilichojaa mafunzo mengi mema yahusuyo kanuni za kimaisha na kitabu cha Mithali kimejaa mafunzo hayo.

Hivyo biblia inatufundisha wakristo tuwe na kiasi katika kulala, kwani usingizi unaozidi una matokeo mabaya.. Si kila changamoto inasababishwa na “wachawi”….. nyingine zinatokana na tabia zetu wenyewe.., na hivyo biblia inatufundisha jinsi ya kuepukana nazo, kwamba ni kubadili tu mienendo.

Maana yake ni kwamba, tukitaka kuepukana na “umasikini”  kanuni sio tu “kufunga na kuomba” bali pia ni KUTOUPENDA USINGIZI!. Ukifunga na kuomba na huku unaendekeza usingizi kupita kiasi hakuna matokeo yoyote utakayoyaona.

Maana yake kama ni mfanyakazi basi usiwe mtu wa kupenda kulala mno..Ni kweli hatuwezi kuacha kulala kabisa, lakini kusizidi mipaka, kwani usingizi uliozidi ni zao la ibilisi.

Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”

Lakini pia kiroho hatupaswi kulala kabisa, kwani usingizi wa kiroho matokeo yake ni mabaya kuliko ule wa kimwili.. Matendo yote ya giza mtu ayafanyayo ni matokeo ya usingizi wa kiroho..

Mtu anayefanya uzinzi, uasherati, anayelewa pombe, anayeiba, anayetukana, anayesengenya…huyo macho yake yamefumba kwa usingizi mzito.

Je na wewe umo miongoni mwa waliolala kiroho? Basi huu si wakati wa kuendelea kulala, bali wa kuamka na kuyaacha matendo ya giza.

Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba SAA YA KUAMKA KATIKA USINGIZI imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini

12  USIKU UMEENDELEA SANA, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.

13  Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”

Waefeso 5:14 “ Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza

15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16  mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.

Bwana atubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.

NYOTA YA ASUBUHI.

Nini maana ya usijiongezee hekima mno? (Mhubiri 7:16b)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments