Epafrodito ni nani kwenye biblia?

Epafrodito ni nani kwenye biblia?

Epafrodito alikuwa ni mmoja wa watendakazi wa makanisa yaliyokuwa Filipi. Anajulikana kama mhudumu wa mahitaji ya mtume Paulo. Tunaona upendo wa Kanisa la Filipi jinsi lilivyomkumbuka Mtume Paulo alipokuwa kifungoni Rumi. Hivyo likaazimu kumtumia mahitaji yake ya kifedha. Ndipo likamchagua huyu Epafrodito. Kusafiri umbali wote huo mrefu na kiasi hicho kingi cha fedha mpaka Rumi.

Wafilipi 4:18  Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.

Na jambo hili lilikuwa ni desturi yao, kumtimizia Paulo mahitaji yake mara kwa mara (Wafilipi 4:16)

Lakini tunaona mbeleni katika waraka wa Paulo, anaeleza hali ya ndugu huyu ambaye Paulo  alimwita pia mtume,jinsi ilivyobadilika kwa kuugua sana karibu na kufa, akiwa katika kazi hiyo hiyo ya kumuhudumia Paulo. Lakini  Ijapokuwa alikuwa katika hali mbaya bado hakuacha kumuhudumia Paulo,

Tunasoma katika hali yake ngumu ya kuumwa, Mungu alimhurumia akamponya. Hatujui aliugua ugonjwa gani, lakini ni ugonjwa uliomdhoofisha kwelikweli, kiasi cha kudhaniwa ‘huyu ni wa kufa tu’, na bila shaka ulikaa ndani yake muda mrefu.

Lakini alipomaliza huduma yake, Ndio tunaona Paulo anawaandikia wafilipi waraka huo, na kuurejesha kwao kwa mkono wa huyo huyo Epafrodito,na ndani yake akielezea pia, shida zilizomkuta.

Wafilipi 2:25  Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.

26  Kwa kuwa alikuwa na shauku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi.

27  Kwa maana alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni.

28  Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma, ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu.

29  Mpokeeni, basi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.

30  Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akaponza roho yake; ili kusudi ayatimize yaliyopungua katika huduma yenu kwangu.

Ni nini tunajifunza kwa mtumishi wa Mungu huyu?

Upendo wa kujali hali za wengine. 

Biblia inasema upendo hautafuti mambo yake wenyewe (1Wakorintho 13). Alikuwa tayari kufa, ili askari mwenzake asikose mahitaji yake. Si ajabu Paulo alimwita mtume. Mungu anathamini sana, utume wa namna hii.

Lakini Tunajifunza huruma ya Mungu ijapokuwa alikuwa karibu na kufa, bado Mungu aliweza kumponya akawa mzima kabisa. Hata mimi na wewe, je tunaweza kufikia hatua mbaya ambayo hata madaktari wanasema haiwezekani kupona? Kama ndio mkumbuke Epafrodito, una hali ngumu unayoweza kusema hapa sivuki, mwisho umefika? Mkumbuke Epafrodito. Yote yanawezekana kwa Mungu.

Ikiwa ni mtumishi wa Mungu, usiohofu uteterekapo kiafya au kihali, Mungu anakuona, atakutia nguvu, usiache kumwamini.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

USIFE NA DHAMBI ZAKO!

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments