Bwana Yesu karibu na kuondoka alizungumza maneno haya;
Yohana 14:1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Kwa mara ya kwanza anawafunuliwa wanafunzi wake, kuhusu mambo yaliyo kwa Baba yake tuliyoandaliwa sisi. Na hapo anasema huko kuna “makao mengi”. Hasemi kuna “kao”kana kwamba ni moja, bali “makao” tena mengi.. Hatujui idadi labda ni mia, au elfu, au milioni, au bilioni. Yesu kusema mengi, amini ni mengi kwelikweli.
Ndio maana kumaliza mambo mema Mungu aliyotuandalia inahitaji umilele.
Sasa kibiblia tumepewa kuyajua makao ya aina tatu tu.
Moja, alituletea tayari, Lakini Mengine mawili yatakuja baadaye.
Kao la kwanza: Lilikuwa ni yeye kutukaribisha ndani yake.
Hilo lilitimia muda mfupi sana, baada ya kuondoka, Tunaona baada ya siku 10, siku ile ya pentekoste, alirudi tena juu yetu kama Roho Mtakatifu. Akaingia ndani yetu, Kwa mara ya kwanza sisi ndio tulipokea mahusiano binafsi ya moja kwa moja na Mungu, tukaingia nyumbani mwake.
Matendo 2:1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Mtu aliye na Roho Mtakatifu, huishi tofauti na mtu ambaye hana Roho. Kwasababu ulimwengu wake ni mwingine kabisa na ule wa kwao, Kao lako ni kuu zaidi ya kao lao la kidunia. Raha na pumziko analolipata, walimwengu hawawezi kulipata. Hekima na upeo ulionao wewe,wale hawana, Hakika kao hili ni zuri sana. Unapojazwa Roho vema, ndio unaona uzuri wa kao hilo maishani mwako.
Kao la pili: Ni kao la roho zetu.
Kumbuka roho hizi zipo ndani ya miili hii ya mavumbi. Lakini Yesu aligundua udhaifu wa miili hii hivyo, alikwenda kutundalia miili ya utukufu itokayo juu, ambayo hiyo tutavishwa, siku ile ya unyakuo itapofika, miili ambayo haijatengenezwa kwa malighafi za duniani, bali zile za kimbinguni. Miili isiyozeeka, isiyougua, isiyo sikia njaa, wala isiyokufa. Haleluya. Ni kao zuri ambalo hakuna hata mmoja wetu anapaswa alikose.
2Wakorintho 5:1 Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
2 Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;
3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.
4 Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
Kao la Tatu: Ni mazingira mapya ya watakatifu, ndio ile mbingu mpya na nchi mpya.
Na ule mji wa kimbinguni, Yerusalemu mpya ishukayo kutoka juu kwa Baba. Uzuri ulioko huko hauna kifani. Ni mji unawaka na kumeta-meta utufukufu wa Mungu.
Ufunuo 21:15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.
16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.
18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.
19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;
20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.
21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.
23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.
24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.
26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.
27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo
Haya ni matatu tu! Vipi kuhusu hayo mengine ambayo hatujafunuliwa? Ukiyajua hayo, hutauchukulia wokovu kirahisi-rahisi, utafanya bidii uingie ndani ya Kristo. Mfuate Kristo akupe uzima wa milele. Ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi wasiliana nasi kwa mawasiliano unayoyapata mwisho wa makala hii, bure
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.
About the author