Je Daudi aliwachukia viwete na vipofu? (2Samweli 5:6-9)

Je Daudi aliwachukia viwete na vipofu? (2Samweli 5:6-9)

SWALI: Je Daudi aliwachukia viwete na vipofu? Kama tunavyosoma katika 2Samweli 5:6-9. Je! habari hiyo tunaielewaje?


JIBU:

2 Samweli 5:6-9

[6]Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.

[7]Lakini Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi.

[8]Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani.

[9]Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani.

Habari hii inazungumzia wakati ule ambao Daudi alikwenda kuiteka Yerusalemu na kuufanya kuwa mji wa Mungu.

Alipofika na kukutana na wenyeji wa mji huo, walimdharau na kumsema kimafumbo kwa kauli ya mzaha kumwambia “Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe;”

Wakiwa na maana vita yake ni ya kupambanishwa na watu dhaifu kabisa wa mji, mfano wa vipofu na viwete, hao ndio apambane nao, lakini sio majemedari wa nchi ile. Akiweza hao walau ndio aingie sasa kujaribu kuuteka, huku wakijua kuwa hata hilo Daudi hataweza kwasababu walimwona ni dhaifu.

Na ukweli wakati huo Daudi hakuwa na nguvu yoyote, kwasababu ndio kwanza ametoka kuupokea ufalme. Hawakujua kuwa nguvu zake tangu zamani zina Mungu, ndio zile zilizomwangusha Goliathi ni silaha zake kwa jiwe moja.

Lakini Daudi aliipowafuatia na kuwapiga, na kuwaangamiza, naye alitumia pia jina hilo hilo la vipofu na viwete kimizaha akiwaita wayebusi waliomwonyeshea dharau..pamoja na hilo Daudi alionyesha kuwachia sana.

Lakini mistari hiyo hakumaanisha kuwa anawachukia viwete na vipofu. Hapana Kama ingekuwa hivyo asingemkaribisha Mefiboshethi mtoto wa Yonathani katika nyumba yake ya kifalme kuketi mezani pake daima..(2Samweli 9). Na ikumbukwe kuwa Daudi alikuwa anamcha Mungu na kuwakumbuka sana wanyonge.

Lakini pale inaposema….

“Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani”.

Ni kwamba kufuatana na Daudi kuwasema viwete na vipofu akiwarejea wayebusi, ukazuka msemo huo, ‘vipofu na viwete hawana ruhusu kuingia nyumbani mwa Mungu;. Lakini haikuwa hivyo’..

Misemo na namna hii ilikuwepo tangu zamani hata kuhusu ile habari ya mfalme Sauli, ya kutabiri (1Samweli 19:24), na kuhusu ike habari za mtume Yohana, pale wale mitume wengine waliposikia Kauli ya Bwana Yesu inayosema ikiwa nataka huyu awepo mpaka nijapo, wakadhani kuwa Yohana hata onja mauti kamwe, mpaka Yesu atakaporudi kumbe hawakumuelewa Bwana Yesu, hakumaanisha vile.(Yohana 21:22-23)

Na ndivyo ilivyodhaniwa kwa Daudi kwamba anawachukia vipofu na viwete, kumbe aliwamaanisha wayebusi.

Lakini ni nini hasaa tunaweza jifunza..katika tukio hilo?

Ni kawaida ya adui yetu anapokaribia kushindwa hunyanyua ujasiri wake kwa kiwango cha juu sana. Mji ambao uligeuzwa kuwa wa Bwana, na mwema kuliko yote, ulitanguliwa na dhihaka nyingi za kukatisha tamaa. Hata ukuta aliokuwa anaujenga Nehemia, ambao sehemu yake iliendelea kudumu kwa mamia ya miaka mbeleni ulitanguliwa na dhihaka nyingi za kuvunjishwa moyo. wakisema hata mbweha akipita juu yake utaanguka.

Silaha hiyo hiyo anaitumia adui leo, unapoona maono makubwa ya kuitenda kazi ya Bwana ndani yetu, vitisho vya adui huanzia hapo, aah wewe huna upako, wewe huwezi kuhubiri, huna pesa, huna elimu ya kukutosha, huna uzoefu, utafungwa..hizo zote ni dhihaka, Daudi alishazitambua toka kwa Goliathi, ndio maana akawashinda wayebusi.

Hivyo ni kusimama imara kuitetea injili, kwa imani tukijua hakuna linaloshindikana kwake yeye aaminiye. Na palipo na dhihaka nyingi ndipo palipo na mafanikio makubwa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Wayebusi walikuwa ni watu gani?

Hanithi ni nini katika biblia? (kumbukumbu 23:17)

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments