SWALI: Nini maana ya Mithali 28:28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.
JIBU: Mithali hii hulenga hasaa watawala, iwe ni serikalini, kwenye mataasisi, makanisa n.k. endapo waongozao ni waovu, basi hufanya hata watu (hususani wale wema) kujificha, Au kutoonekana kabisa.
Ndio kama ilivyokuwa katika kipindi cha mfalme Ahabu, alipoiharibu nchi yote ya Israeli kwa kuweka miungu migeni, akichochewa na mkewe Yezebeli. Wakati huo Manabii wengi wa Mungu waliuliwa, na wale waliosalia walijificha wasionekane kabisa, wakabakia tu makuhani wa baali na wenye dhambi. Kiasi kwamba Eliya akadhani ni yeye tu peke yake nabii aliyebakia Israeli. Kuonyesha ni jinsi gani wenye haki, walivyokuwa adimu wakati huo. Lakini Mungu alimwambia Eliya, nimejisazia watu elfu saba wasiopigia goti baali.
Warumi 11:3 Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu. 4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali. 5 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema.
Warumi 11:3 Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu.
4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali.
5 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema.
Ni kama leo tu ulimwenguni, tunavyoona kiwango cha watenda maasi na maasi kinavyozidi kuongezeka, ndivyo inavyokuwa ngumu kukutana na watakatifu halisi, na hiyo inaweza pelekea pengine ukajidhani mpo wachache, au hakuna kabisa kama wewe.
Ukiwa katika mazingira kama haya usipumbazike, ukafanana na ulimwengu. Bali fahamu kuwa wapo, isipokuwa Mungu amewaficha tu. Siku watakapoondolewa waovu duniani ndipo utajua kuwa Mungu anao watakatifu wake, wengi.
Ndio maana ya hilo neno Bali “waangamiapo wasio haki, wenye haki huongezeka”.
Binti ambaye unatembea kwa kujisitiri barabarani, na huwenda huoni aliye kama wewe mtaa mzima, usife moyo, ni kwasababu wasio haki ni wengi. Kijana uliyeamua kuishi maisha ya mbali na uzinzi na anasa usijidhani upo peke yako, songa mbele tambua, ni Mungu amewaficha tu watu wake.
Kwasababu ni Neno la kweli kabisa wasio haki wastawipo, wenye haki hujificha, (sio kwamba wamekufa, bali wapo). Wakati utafika waovu wataondolewa, na sisi tutamiliki na kuangaza. Usiwe mfauta wimbi, nyakati hizi ni za hatari. Ni sawa na kichuguu tu, waweza kudhani hakina kumbikumbi ndani, kina huoni chochote kinachotoka humo, lakini wakati wa mvua, unastaajabia wingi wao umetoka wapi. Vivyo hivyo na wewe endelea kutembea kwa ujasiri katika wokovu wako. Unyakuo umekaribia. Tambua Bwana analo jeshi lake.
Mithali 28:28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Miungu wasio na kikao pamoja na wenye mwili.
Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani.
Semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; (Luka 17:10)
Rudi Nyumbani
Print this post