Wasihiri ni akina nani?

Wasihiri ni akina nani?

Danieli 2:2
[2]Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme.

Wasihiri ni kundi la wachawi, lililojikita kwenye mazingaumbwe. Linatumia uchawi kubadili vitu kwa hila, mbele ya macho ya watu kuwafanya waone kama ni muujiza umetendeka, na wakati mwingine kutumia njia hiyo kuleta madhara kwa watu.

kwamfano wale yane na yambre kipindi cha Musa walikuwa ni wasihiri, walijaribu kubadili fimbo kuwa nyoka, na kuleta vyura.(Kutoka 8:7)

Mfano mwingine ni yule Simoni mchawi, tunayemsoma katika;

Matendo 8:9-11

[9]Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.

[10]Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.

[11]Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.

Tofauti na waganga ambao, wenyewe wanajifanya kama matabibu, na wachawi na wale wakaldayo ambao ni wanajibu(wasoma nyota)…hawa wasihiri kazi yao hasaa ni ile ya kiini macho.

Lakini Mungu anathibitisha kwamba makundi yote haya, hakuna hata moja lenye uwezo wa kufikia hekima ya Mungu ipitayo vyote Hayana nguvu ya kupambanua mambo. au kufanya miujiza. Hakuna mganga wala wachawi, mwenye uwezo wa kufanya muujiza.

Sasa utauliza ni nini kile wanachokifanya kama sio miujiza?

Awezaye kutenda miujiza ni Mungu tu. wasihiri na waganga wanafanya kazi ya kulaghai fikra za watu kwa elimu ambayo ni ya siri (ya mashetani), ndio maana wanaofanya hizo kazi huenda kujifunza kufanya hivyo, namna ya kuchezea fikra za watu, na si kingine.

Sasa wewe kwasababu hujaijua hiyo elimu unaweza ukasema umeona muujuza kumbe ni uongo tu..wamekudanganya.

ni sawa na leo unapoona mtu akiwasiliana na mtu mwingine akiwa mbali na kuiona sura yake kwenye kioo, kama huijui elimu ya darasani, utasema ni muujiza lakini kumbe ni maarifa tu ya kibinadamu.

vivyo hivyo na hawa wachawi na wasihiri, hawana jipya kusema wanafanya muujiza fulani, ni elimu zao tu za kipepo

Hawawezi kuumba chochote. wale vyura waliofanya kutokea kipindi cha Farao, hawakuumba vyura wao wapya kimiujiza..Vinginevyo mpaka leo shetani angekuwa na uwezo wa kuumba na angeumba vyura wake wengi tu na viumbe vyake vimwabudu. Alichokifanya pale ni kuchukua vyura walioumbwa na Mungu, na kuwapumbaza watu macho, waone ni mawe yamegeuzwa vyura kumbe hakuna kitu. Ndio maana ujinga wao ulikuwa wazi baadaye…walipodhani kila eneo ni kiini macho, walipojaribu kwa chawa wakashindwa, kibao kikawageukia, wakakiri ni Mungu tu awezaye.

Kwahiyo wewe uliye na Yesu, shetani anakuona kama mungu duniani, mwenye nguvu nyingi sana, hekima mamlaka zaidi ya yeye. Wewe unaweza kutenda muujiza kabisa kwa jina la Yesu. yeye hawezi

mwamini Yesu mtegemee yeye tu, kwanini kutafuta msaada kwa vitu dhaifu, ukamtia Mungu wivu?. Kwenda kwa waganga ni kupungukiwa akili, ni kujitenga na fadhili zako, mwenyewe, ni kumdharau muumba wa mbingu na nchi, Yehova, atupaye vyote.

Okoka sasa, mpokee Yesu, upate uzima wa milele. Wachawi waliokutana na Yesu walisalimu amri na kuchoma mikoba yao. sasa wewe unaenda kufanya nini huko?

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).

 

JIHADHARI NA ROHO YA YEZEBELI.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments