Swali: Je Mungu anaua kama watu wanavyoua?
Jibu: Ndio Mungu pia anaua, maandiko yanasema hivyo..
Mathayo 10:28 “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; AFADHALI MWOGOPENI YULE AWEZAYE KUANGAMIZA MWILI NA ROHO PIA KATIKA JEHANUM”
Sasa anayeweza kuua mwili na kuungamiza kwenye jehanamu ya moto ni MUNGU peke yake, mwanadamu anaweza tu kumuua mtu, lakini asiweze kuiona roho ya mtu wala asijue inakokwenda, lakini Bwana MUNGU anaweza kufanya yote (kuua mwili na kuangamiza roho vile vile)
Na maangamizi ya MUNGU ni makubwa na mabaya sana kwani hasira yake iwakapo haangalii wingi, ndicho kilichotokea wakati wa gharika ya Nuhu, dunia nzima iliuawa isipokuwa watu nane (8) tu ndio waliosalimika, na aliyewaua si shetani bali ni MUNGU mwenyewe.
1Petro 3: 20 “watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
Na Bwana MUNGU anaua mtu/watu pale maovu/maasi yanapozidi sana, kiasi kwamba watu hao hata maonyo hawataki kusikia tena..
Kutoka 22: 22 “Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.
23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
24 na hasira yangu itawaka moto, NAMI NITAWAUA NINYI KWA UPANGA; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima”
Maandiko mengine yanayoonyesha kuwa Mungu anaweza kuua ni pamoja na Amosi 2:3 na Ufunuo 2:23.
Lakini pamoja na kwamba Mungu ni mwingi wa hasira na pia anaua, na maangamizi yake ni makubwa na mabaya kuliko ya wanadamu, lakini bado yeye NI MWINGI WA REHEMA WALA SI MWEPESI WA HASIRA.
Nahumu 1:3 “Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi,…”
Hasira yake ipo mbali sana, na iko hivyo ili tupate nafasi ya kutubu kabla ya hasira yake kumwagwa.
2Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea”
Je umempokea Bwana YESU au bado unajitumainisha na mambo ya mwilini, yaletayo hasira ya Mungu?..
Warumi 8: 13 “kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi”
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.
NIFANYE NINI NIWEZE KUDHIBITI HASIRA?
Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu?
About the author