ANZA MWAKA NA KUSAMEHE

ANZA MWAKA NA KUSAMEHE

Maandiko yanasema Makwazo hayana budi kuja (Luka 17:1)

Unapofanyiwa jambo baya na Mtu wako wa karibu au wa Mbali, huwa ni ngumu kusahau…

Kama umeshaokoka na ni mtu uliye mwepesi kusamehe na kusahau, basi Bwana amekutengeneza kwelikweli na umetengenezekeka, Lakini kama ndani yako kuna UGUMU wa kusamehe, fahamu kuwa hilo ni tatizo ambalo unapaswa ulitafutie ufumbuzi haraka sana, mwanzoni mwa mwaka.

Umeumizwa na Ndugu, umeumizwa na Mpendwa mwenzako, umeumizwa na Rafiki, umeumizwa na Mke, Umeumizwa na Mume, umeumizwa na watoto, mchungaji, mshirika wako, mkufunzuki wako au mtu mwingine yeyote, leo itoe hiyo sumu..

Fanya jambo  hili  moja ili ushinde hali hiyo ya kutokusamehe na hatimaye uachilie msamaha.

UTAFAKARI MSAMAHA WA YESU.

Tafakari ni mambo mangapi mabaya uliyoyafanya au unayoyafanya kwa MUNGU, unaweza ukawa hujawahi kumfanyia mtu ubaya, lakini vipi MUNGU?.. Je hujawahi kumfanyia ubaya kabisa?..huna dhambi kabisa??, huna kasoro kabisa??.. Hilo ni jambo lisilowezekana. (2Nyakati 6:36)

Tafakari tu mawazo yako kwa siku yanavyo vuka na kuwa machafu, na MUNGU anakutazama tu!, tafakari ni vipindi vingapi umewaka hasira moyoni na Mungu anakutazama tu, tafakari ni mangapi amekusamehe, na ni mangapi unayohitaji ukusamehe.

Hayo yote uliyoyafanya na unayoyafanya Mungu anayatazama tu, na yupo tayari kukusamehe, au huenda ameshakusamehe, sasa kama wewe umesamehewa mengi hivyo bure kabisa, vipi na wewe kwanini usimsamehe yule aliyekokosea mwaka jana, au mwezi jana, au siku ya jana??.

Wakati mwingine si lazima yeye akuombe msamaha,  Wewe samehe tu hata kama hajaja kukuomba msamaha, maana hata BWANA aliwasamehe wale wasiomwomba msamaha..

Luka 23:34 “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.

35  Watu wakasimama wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake.”

Wengine watakukosea na daima wataendelea kujiona wapo sawa, na wengine wataendelea kukukosea  tu!.. Lakini kanuni ni ile ile KUSAMEHE..

Hivyo kwa kuutafakari mambo ya maisha yako, na kasoro zako mbele za MUNGU, Huwezi kukosa sababu za wewe kutosamehe.

Kwa kumalizia hebu tafakari kwa undani maandiko yafuatayo…

Mathayo 18:21  “Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?

22  Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

23  Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.

24  Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.

25  Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.

26  Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

27  Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.

28  Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata,akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho.

29  Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

30  Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.

31  Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka”.

Kumbe tusipokuwa na TAFAKARI ya kutosha kwa msamaha BWANA aliotupa, yaweza kuwa sababu ya sisi pia kutosamehewa!. Lakini kama tukifakari kwamba na sisi tumeshafanya mengi mabaya, ambayo hayakustahili msamaha basi na sisi pia tutasamehe.

Mhubiri 7:20 “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.

21 Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.

22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine”.

Mwombe Bwana katika mwanzo wa mwaka huu akuumbie  “Moyo wa kusamehe”.. Ni yeye ndiye anayetoa huo moyo, ikiwa tutamwomba, kwa kumaanisha kabisa, Hivyo jifungie chumbani kwako, au tafuta sehemu yoyote yenye utulivu na mwambie Bwana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TAFAKARI SANA KABLA YA KUAMUA HATIMA YAKO.

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.

Maana ya Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake.

Je! Kiongozi wa dini anaouwezo wa kusamehe dhambi?

BWANA ANASAMEHE.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments