Kichwa cha waraka huu kinasema. “ Waraka wa pili wa Paulo mtume kwa Wathesalonike”
Kutuonyesha kuwa Paulo ndiye mwandishi wa waraka huu, kwa kanisa hili la Thesalonike.
Lakini pamoja na hilo tunaona Waraka huu wa pili kama ulivyo ule wa kwanza anawataja pia Timotheo na silwano(Sila), kama waandishi wenza.
Aliundika akiwa Korintho, sawasawa na taarifa tunazozipata katika kitabu cha Matendo 18,.
Maudhui makuu ya waraka huu yalikuwa ni matatu(3), nayo ni;
Kwa maelezo mafupi tuyaangazie maeneo hayo matatu.
> Paulo anawatia moyo watakatifu kwa uthabiti wa imani yao ambayo imesimama sikuzote hata ilipopitia kwenye dhiki nyingi na adha.
2 Wathesalonike 1:4
[4]Hata na sisi wenyewe twaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya saburi yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
> Lakini pia anawaeleza hatma ya watu wanaowaletea adha, kwamba Mungu ni wa haki, na atawalipiza kisasi hao wanaowatesa. Kwa kuwaadhibu kwa maangamizi ya milele.(1:8-9)
2 Wathesalonike 1:6
[6]Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;
> Lakini anaeleza ahadi ya raha ambayo Mungu amewawekea waamini huko mbeleni watesekao kwa ajili yake.
2 Wathesalonike 1:7
[7]na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake
Anarekebisha upotofu uliozuka juu ya siku ya Bwana,kama kweli tayari imeshakuwapo au la, hivyo katika sura hii ya pili, anawaonya kwa kuwaambia siku hiyo haiji kabla ya ule ukengeufu kwanza kuja, na yule mwana wa kuasi, mwana wa uharibifu (mpinga-kristo) kufunuliwa.
2 Wathesalonike 2:1-3
[1]Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,
[2]kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.
[3]Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
Akiwa na maana kuwa kabla ya Kristo kurudi mara ya pili, ukengeufu wa kiroho mkubwa sana utatokea, na yule mpiga-kristo kujidhihirisha na kujulikana kwa kazi zake.
Ambazo zitakuwa ni kama ifuatavyo;
> Kujiinua juu ya kila kitu kiitwacho Mungu, akijifanya yeye ndio kama Mungu.
2 Wathesalonike 2:4
[4]yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
> Atakuwa na utendaji kazi wa shetani ndani yake, kwa kufanya maajabu ya uongo ili kuwadanganya wote waliomkataa Mungu katika fahamu zao.(2:9-12)
> Lakini mwisho wake utakuwa ni kuangamizwa na Yesu.(2:8)
Paulo anaendelea kusema kwasasa hawezi kutenda kazi kwasababu yupo azuiaye, mpaka atakapoondolewa.
2 Wathesalonike 2:6-7
[6]Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
[7]Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
Na huyo si mwingine zaidi ya Roho Mtakatifu. Lakini kumbuka Sio kwamba ataondolewa lakini mifumo yake inayozuia utendaji kazi wa mpinga-Kristo itafikia mwisho..Kwamfano kanisa kunyakuliwa, na mifumo ya kiutawala iliyoruhusiwa na Mungu maalumu kudhibiti kazi zake, kuachwa kutumiwa na Mungu, na malaika wanaohuduma duniani kwa ajili ya usalama wa watakatifu, kuondolewa..
Vitu kama hivi vitakapoondolewa basi mpinga-Kristo atapata uhuru wote kutendakazi kwa jinsi apendavyo.
Paulo anawasisitiza watakatifu juu ya kuiombea huduma, ili injili ya Kristo itukuzwe, lakini pia aweze kuepushwa na watu wabaya.
Pamoja na hilo anatoa tahadhari kuhusu uvivu, akiwasisitiza wafanye kazi kwa mikono yao, pengine kwasababu ya ufahamu usio sahihi waliokuwa nao hapo mwanzo, kwamba mwisho tayari umekwisha fika.
Pia anawatia moyo watakatifu wasikate tamaa katika kutenda mema. Huku akiwahiza wadumu katika mapokeo yao tu waliyowaachia, na si mengineyo.
mwisho anamaliza na salamu pamoja na baraka kwa kanisa.
Kwa ufupi tuusomapo waraka huu Bwana anataka tuendelee kuthibiti katika imani,.haijalishi ni dhiki za namna gani tutazipitia.
Lakini pia tuwe na ufahamu sahihi juu ya siku za mwisho. Kwasababu tatizo hili lipo hata sasa, baadhi ya watu wakiamini kuwa siku ya Bwana imeshakuja. Lakini kama tulivyojuzwa hapo, haiwezi fika kabla, mpinga-Kristo kudhihirishwa na hilo litakuwa wazi kabisa duniani kote.
Na mwisho ni wajibu wetu kuombea huduma, na wanaojitaabisha kuhubiri injili ili walindwe na watu wabaya. Je unamwombea mchungaji wako?
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Mwandishi na uchambuzi wa kitabu cha Wathesalonike wa kwanza.
Rudi Nyumbani
About the author