Kwanini Mungu alimchagua Musa, na si mtu mwingine?

Kwanini Mungu alimchagua Musa, na si mtu mwingine?

Mungu hakumchagua Musa kwasababu ya wema, au kipawa, au ujuzi fulani aliokuwa nao tofauti na wengine. Hapana almchagua ili ‘kutumiza kusudi lake la kuchagua’ ambalo tunalisoma kwa urefu katika (Warumi 9:11-17). Linalomaanisha Mungu humchagua mtu na kumfanya awe kama anavyotaka mwenyewe, na sio kwa jinsi Yule mtu atakavyo.  Kwamfano alimchagua Farao, kisha akamwekea moyo mgumu,ili atimize kusudi lake mwenyewe, kujichotea utukufu kwa mapigo yale kumi,aliyoyaachia kwa wamisri, vivyo hivyo na kwa Musa alimchagua na kumpa neema ile kubwa ya hofu ya Ki-Mungu na upole ili atimize kusudi lake la kuwakomboa wana wa Israeli.

Lakini hakuwa na tendo lolote jema alilowahi kutenda lililomshawishi Mungu amchague yeye tofauti na wengine.

Na ndivyo anavyofanya hata sasa kwa wanadamu wote. Tunaokolewa na kutumiwa na Mungu kwa neema tu, na si kwasababu ya matendo Fulani mema tuliyowahi kumtendea Mungu.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini tofauti ya Majira na Wakati?

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA. 

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments