Kwanini Musa alisita kuitikia mwito wa Mungu alipoitwa mlimani?

Kwanini Musa alisita kuitikia mwito wa Mungu alipoitwa mlimani?

Musa alikuwa na sababu kadha wa kadha za yeye kufanye vile, ikiwemo

  1.  Alijiona hastahili

Kutoka 3:11

[11]Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri?

  1. Kutolijua jina lake.

Musa aliogopa, kwenda kuwahubiria watu juu ya Mungu Ambaye hakulijua jina lake, kwani zamani zile, miungu yote ilifahamika kwa majina, hivyo alijiona kama kwenda kuwaambia watu habari za Mungu asiyejulikana jina lake, ni kama anawafedhehi.

Kutoka 3:13 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini?

  1. Kujidhania kuwa watu hawatamwamini.

Kutoka 4:1

[1]Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea.

 Kwasababu alikuwa hana ishara yoyote ya ki-Mungu ndani yake. 

  1. Kutokuwa na ujuzi wa kuongea

Kutoka 4:10

[10]Musa akamwambia BWANA Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.

Pamoja na Mungu kumwakikishia kuwa atakuwa naye na kumsaidia lakini Musa bado akakataa, ndipo Mungu akaghadhibika na kumletea nduguye Haruni, kama msaidizi wake.

Jambo ambalo halikuwa mpango wa awali wa Mungu, kwani uongozi wa Haruni hakuwa kusudi kamilifu la  Bwana. Sababu kadha wa kadha zilizowapelekea wana wa Israeli kupata adhabu, zilikuwa ni pamoja na uongozi dhaifu wa Haruni. Utakumbuka wakati Musa amepanda juu mlimani kuchukua zile mbao mbili za amri  10, Haruni aliachiwa uongozi kwa muda, watu walipomfuata Kwa ajili ya hatma zao, akasikiliza mapendekezo yao akawaundia sanamu ya ndama ili waiabudu, ikapelekea Mungu kuwaangamiza wana wa Israeli wengi sana, (Kutoka 32:1-6) mzizi huo ni kutokana na kutokutii kwa Musa, halikadhalika sababu ya Musa kutoiona nchi ya ahadi ilichangiwa pia na uongozi hafifu wa Haruni, kwani kule Meriba kosa alilofinya Musa la kuchukua utukufu wa Mungu, alihusika na Haruni pia. (Hesabu 20:10-12)

Hivyo ni wazi kama angekuwa na imani na Mungu, mengi yasingetokea mbeleni. Hata wakati huu wa sasa, wengi wetu tumejikuta katika machaguzi ya pili ya Mungu kwasababu tu, ya kumpotezea imani, kuwa anaweza kutenda  kusudi lake lote hata katika Madhaifu yetu.

Mwamini Mungu mtegemee yeye tu.

Shikilia vifungu hivi vikusaidie.

Mithali 3:5

[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

Isaya 6:8

[8]Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.

2 Timotheo 1:7

[7]Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini Mungu alimchagua Musa, na si mtu mwingine?

Je ni sala gani inahitajika kabla ya kumchinja mnyama katika ukristo?

Je maombi ya mlimani yana ulazima wowote kwa mkristo?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments