Mithali 29:9 Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
Mstari huo kwa lugha rahisi tunaweza kuuweka kwa namna hii. “Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu, akijibu kwa kicheko au kwa hasira, matokeo ni yaleyale tu hakuna amani au suluhisho”
Unafunua sifa za mpumbavu, kwamba sikuzote mwitikio wake wowote hauwezi kuleta mabadiliko. Kwamfano labda hoja imetolewa na ikamuumiza kiasi cha kumfanya ajibu kwa hasira. Sasa wewe waweza tarajia pengine jambo hilo limemgusa kweli moyo, litambadilisha lakini matokeo yake ni kwamba anakuwa vilevile, Halikadhalika waweza kutoa hoja ikamfanya acheke ukitarajia kitaambatana na badiliko lolote ndani yake lakini hakuna.
Maana yake mpumbavu, haguswi kwa ukali au kwa wepesi wa maneno ya aina yoyote…Na hivyo ni kuachana naye Tu.
Tukiachia wapumbavu wa kawaida tunaowafahamu..Mpumbavu hasaa ni yule mtu anayeikataa kweli ya Mungu mfano wa wale waandishi na mafarisayo wakati wa Bwana Yesu (Mathayo 23:17), mtu wa namna hii unapomuhubiri injili, hata imchomeje au imchekesheje hawezi kufikiri hata chembe kubadilika, kinyume Chake ni mapambano tu.
Bwana Yesu alitufundisha na kutuambia kuwa si kila mtu ni wa kumtupia lulu zetu, maana yake wanaweza kutugeukia na Kuturarua. Ukiona mtu anaishia kwenye ubishi tu na mashindano, ni kuachana naye na kugeukia waliotayari kupokea.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Elewa tafsiri ya Mithali 27:22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni.
About the author