Je wazo la Herode kutafuta kumuua mtoto YESU lilitoka wapi?

Je wazo la Herode kutafuta kumuua mtoto YESU lilitoka wapi?

Wakati Herode anaua watoto kule Bethlehemu baada ya kuzaliwa YESU je roho iliyokuwa ndani yake ilikuwa inatoka wapi?.. Kama ni shetani, je shetani hakujua kama Yusufu na Mariamu wametoka na wameelekea Misri?.


Jibu: Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa roho iliyokuwa ndani ya Herode ni ya “shetani” na wala hazikuwa akili zake Herode..Kwasababu kitabu cha Ufunuo kinaonyesha wazi kuwa ni Joka (yaani shetani mwenyewe) ndiye alikuwa anatafuta kumwangamiza Bwana YESU wakati anazaliwa na si Herode (Herode alitumika tu kama chombo)

Ufunuo 12:3 “Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

4  Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka AKASIMAMA MBELE YA YULE MWANAMKE ALIYE TAYARI KUZAA, ILI AZAAPO, AMLE MTOTO WAKE.

5  Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi”.

Sasa swali kwanini shetani asiahirishe ajenda yake ya kuua watoto Bethlehemu baada ya kujua kuwa mtoto hayupo tena Bethlehemu?..

Kikawaida uwezo wa shetani si kama wa MUNGU.. MUNGU anaweza kufanya pasipo ushirika na yoyote, na anaweza kufanya jambo likabadilika kwa muda mfupi, lakini si shetani..

shetani anaposhindwa kufanikisha jambo lake lolote baya kupitia mapepo wake, huwa anatumia wanadamu.. kwamfano akishindwa kumuua amtu kimazingara, basi anaweza  kutumia mtu/watu kufanikisha adhimio lake hilo,  hivyo anaweza kuweka wazo ndani ya mtu la kuua, na huyo mtu akaanza maandalizi ya mauaji (jambo ambalo linaweza kuchukua muda mrefu) tofauti na hiyo njia ya kwanza ya kimiujiza-ujiza ambayo ni ya haraka tu ikiwa mtu huyo hana ulinzi wowote wa kiMungu.

Lakini njia ya kumtumia mtu kuua inachangamoto kubwa kwa shetani, Kwasababu ni lazima kwanza amwandae huyo mtu (atakayemtumia kuua), pengine amwekee wivu ndani yake au hasira, na pia amshawishi vya kutosha na kumfundisha njia, sasa mpaka yule mtu aelewe na kutenda kama shetani anavyotaka inaweza kuchukua muda,

Na vile vile si rahisi kulitoa wazo ndani ya mtu (alilokwisha kumwekea), na kubadilisha mpango kwa haraka, kwamfano kama alikuwa amemfundisha mtu aue kwa sumu, na akataka ambadilishie wazo hilo amwekee lingine la kumuua kwa kumchoma kisu, haiwezi kuwa ni jambo la haraka, itamgharimu shetani muda mwingine wa kutosha kufuta wazo la kwanza na kupandikiza wazo la pili ndani ya mtu.

Ndio maana utaona baada ya mtoto kukimbizwa Misri, bado wazo lile la ibilisi ndani ya Herode la kumuua mtoto halikutoka, matokeo yake Herode aliendelea na mauaji….hivyo kubadilisha mpango kwa haraka ilikuwa ni ngumu, zilihitajika taarifa zimfikie Herode kwamba mtoto hayupo kakimbilia Misri, na Herode aamini, na kuahirisha wazo lile.

Kwahiyo shetani alishajua mtoto kakimbilia Misri, lakini kulibadilisha wazo kwenye kichwa cha Herode halikuwa jambo jepesi la dakika moja.

Hiyo pia ikifunua kuwa dhambi ndani ya mtu inayo maandalizi, huwa haiji ghafla, ni lazima kwanza shetani apandikize magugu ndani ya mtu ndipo mwisho aitekeleze, Hivyo ni lazima tuikatae dhambi katika msingi wake, Laiti Herode angeikataa dhambi katika msingi wake pale wivu ulipoingia ndani yake, bila shaka asingeendelea na hatua zinazofuta za mauaji, lakini aliporuhusu wazo la ibilisi lichipue ndani yake ndipo akawa kifaa tosha cha ibilisi.

Vile vile Kaini alionywa na MUNGU, juu ya dhambi ya wivu inayochipuka ndani yake, laiti kama angemsikiliza MUNGU asingefikia hatua ya mauaji, lakini alidharau maonyo ya MUNGU na mwisho akawa kifaa cha ibilisi cha mauaji.

Mwanzo  4:6 “Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 

7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua”.

Vile vile na sisi ni lazima tuikatae dhambi katika uchanga wake, mawazo mabaya yajapo ni wakati wa kuyakataa kabla hayajatupeleka katika matendo, fikra mbaya zijapo ni wakati wa kuzikataa katika uchanga wake, hasira ijapo, chuki zijapo, uchungu ujapo na mambo mengine yote mabaya ni wakati wa kukataa, kama hayajafikia kukomaa..

Vile vile dhambi ikiisha kukomaa ni ngumu kuiacha, ndio maana ilikuwa ni ngumu shetani kumbadilishia Herode mpango kwa haraka, kwasababu tayari ile dhambi imeshikamana naye.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

YULE JOKA WA ZAMANI.

Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments