1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
JIBU: Katika vifungu hivyo biblia inaeleza kwa ukubwa sifa zetu sisi tuliomwamini Yesu Kristo, jinsi zilivyo kuu, anasema sisi ni mzao mteule, na pia watu wa milki ya Mungu. Lakini sifa nyingine ndio hiyo ya ukuhani wa kifalme.
Angeweza kusema sisi ni ukuhani wa kisomi, au ukuhani wa kiroho, au ukuhani ki-mbingu, au ukuhani wa kitajiri. Lakini anatumia Neno ukuhani wa kifalme. Ikiwa na maana kuwa tunao ukuhani lakini si ukuhani tu bali wenye asili ya kifalme.
Sifa kuu ya kuhani, ni kuweza kumkaribia Mungu kusema naye, na kufanya upatanisho kwa ajili ya watu wengi. Mfano wa Haruni na uzao wake. Tunaona hawa tu ndio waliopewa neema ya kuweza kumkaribia Mungu katika kiti chake che rehema, kuzungumza naye na kuomba rehemu kwa taifa zima. Wengine wote walikaa nje ya hema.
Lakini pia sifa ya mfalme ni uweza, mamlaka, nguvu, na utajiri. Mfalme anatawala, mfalme ana nguvu ya kijeshi, mfalme ni lazima awe tajiri na mwenye utiisho.
Sasa tukirudi kibiblia, Haruni na walawi wote ambao waliopewa sifa ya kikuhani, hawakuwa na ukuhani wa kifalme ndani yao. Waliishia tu kukaa hemani, na sio ni makuhani na wakati huo huo ni wafalme, lakini pia wafalme wengi (Mfano wa Daudi, Sulemani n.k.)hawakuwa na ukuhani pia ndani yao.. Hivyo waliishia tu kutawala lakini sio kuingia hekaluni kuvukiza uvumba. Alitokea mfalme mmoja kujaribu kufanya kazi hizo mbili kwa wakati mmoja, aliishia kupata ukoma kwasababu hakukuwahi kutokea mtu mwenye uwezo huo wa kutembea katika vyeo vyote viwili kwa wakati mmoja (2Nyakati 26:16-21).
Lakini yupo aliyetabiriwa na manabii kuwa atakuwa kuhani mkuu lakini pia mfalme. Na huyo si mwingine zaidi ya Bwana wetu Yesu Kristo. (Waebrania 7:11-17), Yeye alikuwa kuhani lakini pia alitokea katika kabila la kifalme la Yuda, kwa jinsi ya mwili.
Na mpaka sasa anatawala kama kuhani mkuu wetu, lakini pia mfalme wetu. Amewazidi makuhani wote, amewazidi wafalme wote.
Hivyo na sisi tuliozaliwa na yeye, tunarithi vyote alivyonavyo, maandiko yanasema hivyo (1Petro 1:3-4), Tunafanyika sio tu makuhani, ambao tunamkaribia Mungu kusema naye ana kwa ana, na kuwapatanisha wengine na yeye, lakini pia tunafanyika wafalme wenye mamlaka yote, na nguvu, na utajiri.
Sisi tumepewa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka, na nguvu zote za Yule mwovu, mamlaka ya kupooza kila aina ya magonjwa na madhaifu, mamlaka ya kufungua na kufunga jambo lolote. Vilevile tumepewa na utajiri wote wa hekima na maarifa ndani ya Yesu Kristo (Waefeso 1:3).
Na zaidi mamlaka ya ufalme tuliyonayo itakuja kudhihirika vema mbeleni kwenye utawala wa miaka 1000 wa amani wa Yesu Kristo duniani. Jinsi tutakavyo milika na kutawala na yeye kama wafalme, na yeye akiwa kama mfalme wa wafalme. (Ufunuo 19:16)
Ufunuo 5:10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Je!, umeipokea neema hii?
Ni nini unachosubiri usimpe Kristo maisha yako? Tafakari ahadi kubwa namna hii unapewa bure, ni nani anayeweza kufanya hivyo? Saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubaliwa na Mungu ndio huu, okoka leo, usamehewe dhambi zako, jina lako liandikwe katika kitabu cha uzima.
ikiwa upo tayari kumpokea Yesu, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini maana ya “Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake” (Isaya 9:6)?.
About the author