Fahamu Maana ya Mithali 15:24 Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu;

Fahamu Maana ya Mithali 15:24 Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu;

SWALI: Nini Maana ya Mithali 15:24?

Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.

JIBU: Hapo yapo mambo matatu,

  1. Mtu mwenye akili.
  2. Njia ya uhai,
  3. Na uelekeo wa njia hiyo.

Mtu mwenye akili ni mtu mwenye uwezo wa kufikiri/kupambanua vema na kufanya maamuzi sahihi katika maeneo mbalimbali ya maisha yake. Hivyo hapo anasema mtu mwenye akili anajua vema kuichagua njia yake ya uhai.

Anasema njia yake hutoka chini kuelekea juu. Kwa lugha ya picha ni barabara iliyopinduliwa na kusimamishwa wima kama ngazi,  na sio mfano wa barabara hizi tulizonazo zilizolala chini, ambazo uelekeo wake ni aidha kaskazini na kusini, au mashariki na magharibi.

Sasa hapa anasema njia yake ya uhai huenda juu, ili atoke kuzimu chini. Akiwa na maana husafiri kutoka kuzimuni kuelekea uzimani juu kwa Mungu.

Hufunua nini?

Safari ya mtu mwenye akili, hufikiri kumtafuta Mungu juu alipo,

Wakolosai 3:1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

Hufikiri ukuaji wa kiroho, atokea hatua moja ya utakatifu kwenda nyingi, kiwango kimoja cha Imani kuelekea kingine kama Kristo (2Petro 1:5-10, Waefeso 4:13). Ni mtu ambaye kila siku anakwenda mbali na njia ya mauti. Mawazo yake yapo juu sikuzote kumjua Kristo na mapenzi yake yote.

Lakini kinyume chake ni ukweli, mtu asiye na akili barabara yake haijasimama wima, bali imelala. Atawaza atoke hatua moja kwenda nyingine lakini hakuna ukuaji wowote au kuongezeka kokote. Huwenda anachowaza tu sikuzote ni kutoka katika umaskini kwenda katika utajiri, kutoka katika kiwango kimoja cha elimu kwenda kingine, kutoka katika cheo kimoja kwenda katika kingine..Hatua zake ni za kidunia tu, akidhani ndio uzima wake upo hapo. Kumbe kapotea njia.

Si kwamba vinapingwa vya dunia hapana, ni vizuri na vinafaa, lakini havina uzima wa milele ndani yake. Ili uwe na akili hakikisha unampokea Kristo, kisha unaanza kukua kiroho, kila siku unafikiri njia ya kuyakimbia machafu ya kidunia. Hapo barabara yako itakuwa umesimama kama ngazi na hivyo utaiponya nafsi yako.

Je! Umeokoka?. Kama ni la! Basi wakati ndio sasa fungua moyo wako mkaribishe Yesu akuokoe hizi ni nyakati za hatari, tubu leo upokee wokovu. Ikiwa upo tayari kumkaribisha Kristo moyoni mwako, basi waweza kubofya hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba. Bwana akubariki. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Maana ya Mithali 29:9 Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha. 

Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)

Biblia inasema nini kuhusu mtu ‘Mwenye kujipendekeza (Mithali 29:5)

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments