Jina la Mwokozi YESU libarikiwe.
Wakati Fulani Bwana YESU aliuona “Mtini” (yaani mti unaozaa matuna aina ya Tini) usio na matunda na matokeo yake aliulaani.
Mathayo 21:18 “Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa.
19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; AKAUAMBIA, YASIPATIKANE MATUNDA KWAKO TANGU LEO HATA MILELE. MTINI UKANYAUKA MARA.
20 Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara?”
Sasa ukifuatilia vizuri hii habari utaweza kufikiri kwamba Bwana YESU alikuwa anaweza kuwa amekosea kuulani.., kwani ule mtini haukuwa msimu wake wa kuzaa matunda…
Hata wewe ukienda kutafuta machungwa kwenye mchungwa nje na msimu wake ni wazi kuwa hutashangazwa pale utakapokuta ule mchungwa hauna tunda lolote.Zaidi sana utashangazwa kama endapo umefika msimu halafu hukukuta machungwa.. Lakini sasa tunasoma Bwana YESU ilikuwa kinyume chake alijua kabisa si msimu wake Mtini kuzaa lakini aliulaani hivyo hivyo.
Sasa kwanini aulaani??
Sababu zipo nyingi, lakini hii yaweza kuwa kuu kuliko zote… ULE MTINI ULIONYESHA SIFA ZOTE ZA NJE KUWA NA MATUNDA lakini haukuwa na matunda! (Maana yake ulikuwa unahubiri udanganyifu).
Unaonaje umewekewa bahasha tatu mbele yako, halafu kati ya hizo bahasha tatu mbili zinaonekana kabisa kwa macho kuwa ndani hazina kitu, lakini moja inaonekana imetuna (kana kwamba ina fedha), halafu unaichagua hiyo iliyotuna kisha ndani unakuta hamna kitu, bila shaka utakwazika na unaweza ukaichana ile bahasha, ili isiendelee kudanganya wengine.
Vivyo hivyo Kristo alijua kabisa ule si wakati wa Tini kwani mitini mingine yote ilikuwa na sifa zinazofanana kwa wakati huo, lakini ajabu ni kwamba huu Mtini mmoja ulikuwa na mwonekano wa tofauti kana kwamba unao matunda, pengine wakati mitini mingine ilikuwa imekauka inapukutisha huu ulikuwa na majani mabichi, ulikuwa unahubiri udanganyifu kwamba unao matunda na kumbe hauna, na ili kuondoa udanganyifu huo suluhisho ni kukatwa/kulaaniwa.
Naam na maisha ya wakristo wengi yamejaa UDANGANYIFU, ni kama wanasifa zote za kuitwa wakristo lakini ukichunguza kwa undani hawana matunda!. Kwa nje wana majina ya kikristo, ni wahubiri, wana biblia nzuri na kubwa, wana nafasi katika kanisa, lakini ndani si wakristo, hawana matunda!, ni watu vuguvugu wale Bwana aliosema atawatapika katika Ufunuo..
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.
Toka katika uvuguvugu, ili kuepuka laana ya KRISTO, kama umekusudia kuwa Moto, kuwa Moto mpendwa, kama umeamua kuchagua baridi maandiko yanasema ni heri uwe baridi kabisa kuliko kuwa hapo katikati, vuguvugu..
Bwana YESU atusaidie sana.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Tafsiri ya Mithali 27:18 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake;
Je Bwana YESU alipanda mlimani na wanafunzi wake baada ya siku sita au nane?
MWISHO WA MAVUNO, NI MWISHO WA DUNIA.
Biblia unapozungumzia kuhusu kupewa jina jipya inamaanisha nini?
About the author