Je ni Petro au Mariamu Magdalene aliyekuwa wa kwanza kutokewa na Bwana YESU?

Je ni Petro au Mariamu Magdalene aliyekuwa wa kwanza kutokewa na Bwana YESU?

Swali: Kati ya Simoni Petro na Mariamu Magdalene ni yupi aliyekuwa wa kwanza kutokewa na Bwana YESU baada ya kufufuka kwake?, kwa maana katika Luka 24:34 tunasoma kuwa ni Simoni ndiye wa kwanza kutokewa na Bwana, lakini tukirudi katika Marko 16:9 tunaona ni Mariamu Magdalene je hii imekaaje?.


Jibu: Turee mistari hiyo..

Luka 24:33 “Wakaondoka saa ile ile, wakarejea Yerusalemu, wakawakuta wale kumi na mmoja wamekutanika, wao na wale waliokuwa pamoja nao,

34 wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, NAYE AMEMTOKEA SIMONI”.

Hapa tunaona anatajwa Simoni, lakini turejee Marko 16:9..

Marko 16:9 “Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, ALIMTOKEA KWANZA MARIAMU MAGDALENE, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.

10 Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia”.

Hapa tunasoma ni Mariamu Magdalena ndiye aliyetokewa kwanza, sasa swali ni yupi aliye sahihi au biblia inajichanganya?..

Jibu ni La! Biblia haijichanganyi na wala haina kasoro yoyote… Sasa kama ni hivyo ni nani aliyetokewa wa kwanza?

Jibu, aliyetokewa wa kwanza na Bwana YESU alikuwa ni MARIAMU MAGDALENE, kama maandiko yanavyoonyesha hapo juu (Marko 16:9).. huyu ndiye aliyekuwa wa kwanza kumwona Bwana kwani baada tu ya kukuta jiwe limeviringishwa mbali na kaburi aliondoka na kwenda kuwafuata akina Petro kuwapasha yaliyojiri, na Petro pamoja na Yohana walipokwenda kaburini kuhakiki hizo taarifa za Magdalene,  walikuta tu vitambaa vya sanda, na walipoondoka ndipo Bwana YESU akamtokea Mariamu Magdalene kama mtu wa kwanza (na saa hiyo akina Petro wameshaondoka).

Yohana 20:1 “Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.

2 Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.

3 Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini.

4 Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini.

5 Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia.

6 Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala,

7 na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake.

8 Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini.

9 Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka.

10 Basi wale wanafunzi wakaenda zao tena nyumbani kwao.

11 Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi.

12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu.

13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.

14 Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu.

15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.

16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu)”.

Hivyo baada ya kumtokea Mariamu Magdalena ndipo akamtokea Simoni Petro, katika tukio ambalo halijarekodiwa katika Biblia.

Kwahiyo Simoni Petro alikuwa ni Mtume wa kwanza kutokewa na Bwana YESU lakini si mtu wa kwanza, aliyekuwa wa kwanza ni Mariamu Magdalena na Simoni Petro anasimama kuwa wa kwanza kati ya Mitume wa Bwana.

Mtume Paulo analiweka hilo vizuri zaidi..

1Wakorintho 15:4 “na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;

5 na ya kuwa ALIMTOKEA KEFA; tena na wale Thenashara;

6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;

7 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote;

8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake”.

Je umempokea YESU?.. Unao uhakika wa kwenda naye mawinguni atakaporudi?… fahamu kuwa tunaishi majira ya siku za mwisho, siku yoyote parapanda ya mwisho inalia na wafu waliokufa katika Kristo watafufuliwa kuungana na walio hai katika Kristo na kunyakuliwa juu, je utakuwa wapi siku hiyo?, ikiwa leo habari ya msalaba kwako ni upuuzi mtupu!.

Neema ya Bwana YESU itusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mariamu Magdalene ni nani. Na hilo jina amelitolea wapi?

MAMBO YA KUJIFUNZA KWA KLOPA NA MKE WAKE!

Nyongeza ya majina ya watu katika biblia

MUONEKANO MPYA WA YESU BAADA YA KUFUFUKA.

UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments