SWALI: Naomba kufahamu Biblia unapozungumzia kuhusu kupewa jina jipya inamaanisha nini?
JIBU: Kazi ya jina sio tu kumtambulisha au kumtofautisha mtu mmoja na mwingine. Bali jina linasimama pia kueleza Wasifa wa mtu,
Hivyo jina la mtu linapobadilika, aidha Wasifa pia hubadilika.
Kwamfano Ibrahimu alipobadilishwa jina kutoka Abramu na Kuwa Ibrahimu ni kwasababu alikuwa anaenda kuwa Baba wa mataifa mengi.(Mwanzo 17:5)
Vilevile Sarai kuitwa Sara. Ni kwasababu anaenda kuwa mama wa mataifa mengi..(Mwanzo 17:15)
Sauli kuwa Paulo kwasababu anaenda kuwa mtume kwa mataifa.(Matendo 13:9)
Vivyo hivyo tunaona Mungu katika maandiko Akijitambulisha kwa majina mbalimbali, lengo sio kuonyesha uzuri au upekee wa majina yake hapana bali kutambulisha wasifa wake.
Kwamfano alipojitambulisha kama Yehova rafa, alisimama kama Mungu mponyaji..Yehova yire Mungu atupaye, Yeshua(Yesu), kama Mungu atuokoaye.
Tukirudi kwa wakati wa sasa Biblia Inatuonyesha kuwa Kristo atakaporudi mara ya pili atakuja na jina lingine jipya. Ambalo ndio tunangojea kuona utukufu wake, mamlaka yake na nguvu zake.
Ufunuo wa Yohana 3:12
[12]Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
Jina hili halitakuwa Yesu,tulitumialo sasa ambalo linawasifa wa wokovu, lililojikita katika kiwakomboa na kuwafungua wanadamu katika mauti na vifungo vya kila namna.
Lakini hilo linalokuja litakuwa ni jina lenye uweza Mwingi, la kifalme, la kiutawala zaidi. Wakati huo Kristo hataonekana tena kama mwanakondoo mpole, asimamaye kutuombea kwa Baba N.k..hapana ataonekana katika taswira mpya kabisa ya kifalme, na zaidi ya hapo (Ufunuo 19:11-16), sawasawa na hilo jina lake litakavyokuwa.
Ndio maana kuna umuhimu sana kuokoka sasa, angali neema na msamaha upo katika jina la YESU, kwasababu atakaporudi mara ya pili,na jina jipya hatajua kusamehe ni nini, bali mambo mengine mapya yatakuwa wanaendelea..Usipookoka leo hakuna wokovu siku ya mwisho.
Vilevile wale watakaoshinda Kristo ana ahidi kuwapa majina mapya ya kipekee, ambayo yatawanafisisha kipekee mbele ya Kristo.
Ufunuo wa Yohana 2:17
[17]Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Ndugu Utukufu Unaokuja wa Kristo ni mkuu sana, ni heri ukose vyote sasa, lakini usikose mbingu Mpya na nchi mpya na ile Yerusalemu mpya ishukayo kutoka kwa Baba mbinguni.
Siku hizi ni za mwisho, unyakuo umekaribia sana. Mambo ya umilele yanakaribia kuanza. Bado unaendelea kung’ang’ana na ya kidunia? tubu leo mgeukie Kristo.
Bwana akubariki.
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.
JE NI LAZIMA KUBADILISHA JINA BAADA YA KUOKOKA?
Nini maana ya “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi”?
About the author