SWALI: Kwanini Yesu akubali ombi la mapepo, na si kuyaamulia adhabu yake mwenyewe, au kuyafukuza kabla hata hayajaongea?
Luka 8:31 Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. 32 Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa.
JIBU: Maneno hayo aliyasema baada ya kukutana na mtu yule aliyekuwa amevamiwa na jeshi la mapepo, yaliyomfanya akae makaburini muda mrefu, bila nguo. Hivyo kama tunavyosoma yale mapepo yalipomwona tu Yesu, kabla ya tamko lolote yenyewe yakamfuata na kuwasilisha ombi lao kwa kusihi sana. Kwamba yawaingie wale nguruwe waliokuwa jirani wakichungwa. Yesu akasiliza ombi lao, akayapa ruhusa. Yakamtoka Yule mtu, na kuwaelekea wale nguruwe, na saa ile ile Yule mtu akawa mzima.
Zipo sababu mbili.
Ni wazi kuwa Bwana alilitafakari wazo lao, na kuona kama lingeweza kuleta madhara yoyote au uharibifu wowote wa mpango wa Mungu. Na akaona kinyume chake ni kuwa kusudi la Mungu litaendelea kuthibitika hata katika ombi lao, kwasababu kutoka kwao na kuwaingia wale nguruwe kisha kwenda kujitupa ziwani. Ilikuwa ni udhihirisho wa wazi kwa watu kuwa mapepo ni halisi, lakini pia yanatabia ya uuaji. Kwamfano kama angemponya tu, bila ishara yoyote, pengine wengine wangesema “aah huyu akili zilimruka tu!” alikuwa na stress zake, au maisha yalimtinga sana, akachizika, hivyo amekutana na mwanasaikolojia mzuri amemweka sawa… Lakini kuona mapepo yale yameruhuisiwa kwenda kuingia viumbe vingine, halafu yakawaendesha ziwani kuwaua, ilikuwa ni ishara bora zaidi ya kazi za Mungu.
Utakumbuka mapepo yenyewe yalimwambia Yesu ‘tuna nini nawe, je umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?’
Mathayo 8:29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
Maana yake ni kuwa mapepo yalijua kuwa walishawekewa wakati wao wa mateso baadaye kule shimboni na atakayekuja kuwapeleka huko ni Kristo. Hivyo hapa yanamkumbusha Bwana asibatilishe mpango huo, na kuwaadhibu mapema.
Pengine hiyo ndio sababu nyingine ya Bwana kutotoa adhabu kali kwao, ni kuwa mpango wa hukumu ungebatilika.
Kitendo cha mapepo kujisalimisha yenyewe kuomba kupunguziwa adhabu, ni kuonyesha mamlaka kuu iliyo ndani ya Kristo. Ambayo hata sasa ipo ndani yetu. Hatufundishwi kuongea na mapepo, bali kuyakemea kwa mamlaka yote. Ambayo yaweza tokea mengine hata kabla ya kukemewa yakaomba yenyewe nafasi ya kupunguziwa adhabu. Hilo linawezekana!
Tumia mamlaka uliyopewa ndani yako. Fukuza pepo wote.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Gengeni ni wapi, wale nguruwe walipoteremkia? (Marko 5:13)
DALILI TISA (9) ZA PEPO KUWEPO NDANI YA MTU.
Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?
About the author