Gengeni ni wapi, wale nguruwe walipoteremkia? (Marko 5:13)

Gengeni ni wapi, wale nguruwe walipoteremkia? (Marko 5:13)

Marko 5:12 “Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.

13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; NALO KUNDI LOTE LIKATELEMKA KWA KASI GENGENI, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini”.

“Genge” linalozungumziwa hapo sio lile linalotengenezwa kwaajili ya biashara za mboga mboga, au matunda..Bali Neno “genge” ni Kiswahili kingine cha “Mteremko wa mwamba”..Ipo miteremko ambayo chini ni udongo, lakini pia ipo miteremko ambayo chini ni mwamba…sasa hiyo ambayo chini ni mwamba, ndiyo inayoitwa “Genge”

Kwahiyo hapo biblia iliposema kuwa wale Nguruwe waliteremkia kwa kasi gengeni, ilimaanisha walishuka kwa kasi katika mteremko huo unaoelekea ziwani.. Na tofauti na miteremko ya kawaida na ile ya miamba..ni kwamba miteremko ya miamba INAKUWA INATELEZA!, kiasi kwamba mnyama au mtu au kitu kikianza safari ya kuelekea huko basi kwa haraka sana kitakuwa kimefika hitimisho…Ndio maana hao nguruwe biblia inataja WALISHUKA KWA KASI…

Kufunua ni jinsi gani mapepo yanavyowapeleka watu mahali ambapo si sahihi, na tena kwa haraka sana…Leo hii mtu akiingiwa na mapepo basi, hitimisho lake litakuwa ni KIFO, kama hayatamtoka. Na hakuna pepo lolote lisilotoka endapo mtu akimaanisha kuamua  limtoke. Kwasababu hakuna lililo kubwa kwa Mkuu wa Uzima Yesu, na zaidi sana miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na si mapepo. Kwahiyo tunazo haki zote za kudai uzima na haki zote za kumpokea Roho Mtakatifu endapo tutamhitaji..

Na kanuni za kupokea Roho Mtakatifu ni hii..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Je umetubu na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu?

Maran atha!

Mada Nyinginezo:

JE UNA MATUMAINI YA KUPATA TENA KILE ULICHOPOTEZA?

Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?

Nini maana ya “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi?”

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

RAFIKI WA KWELI NI YUPI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments