Yuda alimaanisha nini kusema “wokovu ambao ni wetu sisi sote”

Yuda alimaanisha nini kusema “wokovu ambao ni wetu sisi sote”

SWALI: Yuda alimaanisha nini kusema “wokovu ambao ni wetu sisi sote”

Yuda 1:3

[3]Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.


JIBU: Mwanzo mwa waraka huu, mtume Yuda anaanza kwa kusema maneno hayo “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote”

Aliowaandikia waraka huu ni watu wote waliomwamini Yesu, (yaani waliookoka) kwamba wokovu huo ni wao Wote.

Anaandika maneno hayo pengine kutokana na dhana iliyokuwepo ya watu kufikiri kuwa wokovu ni wa jamii ya watu fulani tu.. pengine wayahudi, au waliotahiriwa, au mabwana tu..Hapana

Bali Kristo alikivunja kiambazi chote, ili watu wote wastahili kushirikia neema yake sawasawa.

Wagalatia 3:26-28

[26]Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.

[27]Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

[28]Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.

Jambo hilo kwa mwanzoni lilikuwa ni gumu kupokelewa hata na baadhi ya watakatifu wa Yerusalemu. Utakumbuka walipomwona Petro ametumwa na Roho Mtakatifu kwenda nyumbani mwa Kornelio mtu wa mataifa bado ilikuwa ngumu kupokelewa na wao…kwasababu imani na dini zote walizozijua tangu zamani, zote zilikuwa ni za kitabaka, kibaguzi, kitaifa n.k..na sio za kila mtu.

Kitendo cha Yesu kuwaambia kahubirini habari njema za ufalme kwa mataifa yote, bila kujali lugha, cheo au jinsia hawakuelewa vema..ndio maana siku ile ya pentekoste walikuwepo watu wengi wamekusanyika watu wa kila taifa chini ya jua. Na wote wakajazwa Roho Mtakatifu.(Matendo 2)

Hivyo ujumbe huu ni lazima ukae mioyoni mwetu hata sasa ili tusiwe Na ubaguzi katika kuwavuta watu kwa Kristo, au tusionyeshe upendeleo kwa kundi fulani tu la watu, Mungu hapokei uso wa mwanadamu.. linapokuja suala la wokovu na mema yote ndani yake watu wote wamestahili na ni sawasawa machoni pake, kushiriki vipawa vyote vya Mungu.

Mwingine atasema, huwezi kumjua Mungu mpaka uwe chini ya nabii au kuhani fulani, hilo si sawa..

Lakini jambo lingine la kujifunza ni kuwa ijapokuwa ni wetu sote anasema tuishindanie imani.. kwasababu adui naye yupo kazini kutaka kuwang’oa watu wa Mungu kwenye mstari wa imani ya kweli, na kuwafanya waangukie imani danganyifu, zilizoletwa na watu wanaojiingiza Kwa siri ndani ya kanisa..

Hivyo anaeleza mkristo ni wajibu wake, kuilinda imani yake, kwa kuendelea kudumu katika kuomba, upendo, na kujifunza vigezi halisi vya neema ya Mungu, ili asiigeuze kuwa ndio chanzo cha kuishi kwenye dhambi na uovu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NJIA/BARABARA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

LEO WOKOVU UMEFIKA NYUMBANI HUMU

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments