Je ni kwetu tunatakiwa kumpa kila anayetuomba?

Je ni kwetu tunatakiwa kumpa kila anayetuomba?

Swali: Maandiko yanasema katika Mathayo 5:42 kuwa tumpe kila atuombaye na kila atukopaye tusimpe kisogo?.. Je hata kama mtu ni mzembe na kila wakati anatumia vibaya vile ninavyompa, nina amri ya kumpa mara kwa mara kila atakaponiomba?


Jibu: Turejee hayo maandiko..

Mathayo 5:42 “Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo”.

Haya ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo..ambayo anatufundisha umuhimu wa kutoa na kukopesha watu wote pasipo kuwa na vizuizi vingi, lakini swali ni je! Ni kila mtu anayekuja kutuomba tunapaswa tump kulingana na hilo andiko?

Jibu ni La!.. si kila mtu anayetaka kukopa tuweza kumpa, na si kila anayeomba tunapaswa tumpe!.. Kwasababu zifuatazo.

     1. HUNA HIKO ANACHOKIOMBA.

Kama huna hiko anachokuomba, huwezi kumpa, kwasababu huwezi kumpa mtu kitu usichokuwa nacho au kilicho juu ya uwezo wako, kwamfano mtu anataka kukopa kwako milioni moja, na wewe huna hiko kiasi..hapo huwezi kufungwa na andiko hilo kwamba kila akuombaye unapaswa uumpe!

    2. HAJAKIDHI VIGEZO VYA KUPEWA.

Vipo vigezo vya mtu kupewa kitu, kwamfano mtu anataka kukopa au kuomba pesa ya kwenda kununua pombe, au kwenda kufanya dhuluma au biashara haramu, au kwaajili ya kwenda kutoa sadaka kwa miungu hapo hata kama tunacho hiko kiasi, hatupaswi kumpa wala kumkopesha.

Hata Mungu wetu alituambia tumwombe naye atatupa

Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

Lakini ni huyo huyo Mungu wetu aliyetuambia tena kuwa, tukiomba nje ya mapenzi yake hatupati..

1Yohana 5:14 “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia”.

Yakobo 4:3 “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”.

Kwahiyo na sisi ni hivyo hivyo, ni lazima tuangalie anayekuja kuomba kama amekidhi vigezo.. wengine wanaomba kwaajili ya kwenda kufanya maasi, wengine uhalifu, wengine si makini, maana yake wana hali ya uzembe katika matumizi yao (hawa hawapaswi kurudia kupewa mara kwa mara mpaka watakapobadilika), wengine wanaomba kwa tamaa tu (mfano wa hao pia ni watoto wadogo) n.k

Kwahiyo tukirudi hapo katika hilo andiko Bwana Yesu alilosema kuwa “Kila akuombaye mpe”, tutakuwa tumeshaelewa kuwa si kutoa tu bila kufikiri wala kutafakari kwa kila mtu, bali ni kumpa kila akuombaye ambaye AMEKIDHI VIGEZO VYA KUPEWA!.

Kama mtu amekidhi vigezo vya kupewa nawe unacho hiko kitu, usimpe kisogo, kwasababu ni Mungu aliyemleta kwako huwenda ili amtengeneze na wewe pia upate thawabu, ukimpa kisogo mtu anayekuomba na ilihali unacho hicho kitu, ni dhambi!.. kwasababu uchoyo ni shina la dhambi.

Luka 12:15 “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ipi tofauti kati ya sadaka ya dhambi na sadaka za hatia?

Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)

USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake?

Nini maana ya huu mstari; Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply