Katika agano la kale dhambi ilitokea na kuhesabiwa katika maeneo mbalimbali.
Kwamfano
> Kulikuwa na makosa ya jamii nzima. Yaani taifa zima kuasi. (Kutoka 32,)
> Makosa ya mtu binafsi. Mfano kutenda uzinzi, Wizi, uuaji n.k.
> Makosa ya kuwatendea vibaya wanyonge: Mfano maskini, wageni, mayatima na wajane (Amosi 5:11-12),
> Makosa ya kukaidi sherehe za kidini (Walawi 11-15),
> Makosa ya kuvunja maagano (Yeremia 17:21-23),
> Makosa ya kuabudu miungu mingine (sanamu).
Lakini pia kulikuwa na aina nyingine mbili za makosa..
> Aina ya kwanza ni makosa ya kukusudia
> Aina pili ni yale ya kutokusudia.
Ikiwa mtu alitenda dhambi kwa kutojua, alihesabika kuwa ni dhambi, hivyo alilazimika atoe sadaka ya dhambi. Lakini kama alitenda dhambi ya makusudi kinyume na mwenzake, ili kuondoa kosa Ilipasa atoe sadaka ya hatia.
Aina ya sadaka hizi zinaelezwa kwa urefu kwenye kitabu cha Walawi 4:1 – 5:13
Dhambi za kutokusudia Mfano wake ilikuwa ni kama kuvunja amri bila kujua au kutojua Sheria ya vitu safi au najisi ilivyo. Hivyo mtu alijikuta tu anatenda kwa kukosa ufahamu.
Walawi 4:1-3
[1]BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
[2]Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo;
[3]kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.
Dhambi za kukusudia ni zote ambazo zilitendwa kinyume na mtu mwingine au mambo matukufu mfano wa hizi ni kama kuiba, kusema uongo, viapo Vya uongo, hivyo iliambatana pia na kutoa fidia ya vitu hivyo.
Sio tu kusamehewa bali pia kuweka mambo sawasawa kwa kulipia fidia.
Mfano wa tendo hili, tunaona kwa Zakayo, alipofikiwa na wokovu, alitubu kwa kurejesha mara nne ya vyote alivyodhulumu. (Luka 19:8) huo ni mfano wa sadaka ya hatia.
Katika agano jipya dhambi Zote Za kukusudia na kutokusudia na nyingine zote zinaondolewa na sadaka moja tu ya daima nayo ni DAMU YA YESU (Waebr 9:26, Isaya 53:10, 1Petro 2:24). Hiyo tu ndio inafuta hatia zote.
Lakini pamoja na hayo, sadaka hizi hutukumbusha pia kila tuombapo rehema, (kwa unajisi tunaojitia kila siku), hatuna budi kuomba sio tu kwa dhambi tuzijuazo bali pia kwa zile tusizozijua.
Kwasasa dhambi tusizokusudia ni kama vile kumkwaza mwenzako bila kufahamu, Kutowaombea wengine(2Samweli 12:23), kuwaza vibaya, kutotumiza nadhiri zetu, au wajibu wetu N.k.
Bwana akubariki.
Je umesamehewa na kuondolewa dhambi zako? Kama ni la! basi wakati ndio sasa, unapomgeukia Bwana Yesu, anakuondolea kumbukumbu lote la makosa. Hivyo fungua hapa kwa msaada huo wa kumpokea yeye >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).
Nini maana ya dhabihu na matoleo hukutaka? (Waebrania 10:5).
Kwanini Mungu aliikubali sadaka ya Yeftha ya kumtoa binti yake kafara?
About the author