SHUKA UPESI

SHUKA UPESI

Luka 19:1 “Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake.

2 Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri.

3 Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo.

4 Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile.

5 Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, SHUKA UPESI, KWA KUWA LEO IMENIPASA KUSHINDA NYUMBANI MWAKO.

6 Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha”.

YESU hawezi kuingia nyumbani kwako kama “hutashuka kwenye Mkuyu”..

Mkuyu ni kitu chochote kijiinuacho juu ya  YESU,…. Kiburi cha mali ni mkuyu,… kiburi cha cheo ni mkuyu, kiburi cha uzuri ni Mkuyu n.k.. Mtu anavyovitumia hivi ili kumwona Bwana YESU au kumtumikia, Kristo yeye anaenda kinyume navyo..

Zakayo asingeweza kuzungumza na Bwana akiwa juu ya mkuyu..ilimpasa ashuke upesi… Sauti ile ilikuwa na mamlaka, ilipenya katika moyo wa Zakayo na kumfanya ashuke si tu chini ya Mkuyu, bali hata kiburi chake chote, kwani alikuwa ni mtu mkubwa kifedha…

Alipokubali  tu kushuka na kiburi chake cha mali nacho kikashuka, kiburi chake cha cheo kikashuka akawa mtu mwingine, mnyenyekevu na YESU akaingia nyumbani mwake..

Nusu ya mali yake aliwapa maskini na wote aliowadhulumu aliwarudishia mara nne.

Luka 19:6 “Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha.

7 Hata watu walipoona, walinung’unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.

8 Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang’anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.

9 Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.

10 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea”.

Na wewe leo, shuka chini ya Mkuyu.. kiburi cha Elimu kinaweza kuwa kizuizi cha Kristo kutembea na wewe, kiburi cha pesa kinaweza kuwa kikwazo cha YESU kuingia kwako, kiburi cha cheo na uzuri ni hivyo hivyo, lakini unyenyekevu unaleta Neema.

Yakobo 4:6 “Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NINI MAANA YA KUTUBU

ALIYOKUTANA NAYO YESU, YERIKO.

JE YESU AMEJIAMINISHA KWAKO?

LEO WOKOVU UMEFIKA NYUMBANI HUMU

JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments