Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).

Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).

Jibu: Turejee,

Matendo 21:25 “Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati”


Vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu ni vyakula vyote vinavyotolewa kwa maagizo ya kishetani.
Mfano wa vyakula hivyo ni vile vya kimila au vya waganga wa kienyeji.

Mfano wa vya kimilia ni vile ambavyo mtu anakula au analishwa kwa lengo la kumkinga na madhara fulani ya kiroho kama uchawi au kumpatanisha na roho fulani..


Ndio hapo utakuta mtu anaambiwa alete mbuzi, au kondoo na kisha yule kondoo achinjwe kama sadaka/kafara kwa mizimu na kisha ale sehemu ya nyama ya huyo mnyama aliyetolewa sadaka… Sasa endapo mtu huyo akila hiyo nyama au sehemu ya hiyo nyama tayari anakuwa amekula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.


Au utakuta mtu anaenda kwa mganga wa kienyeji na yule mganga anamwambia ili tatizo lake litatulike basi alete mnyama fulani aidha mbuzi, au ng’ombe au kuku na achinjwe kama kafara na nyama yake au damu yake inywewe na mhusika.. Mtu anayekula hiyo nyama anakuwa tayari amekula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.


Au anaweza asiambiwe alete mnyama, bali akaambiwa alete hata nafaka fulani na kisha ile nafaka ikatolewa kwa miungu na mtu akaambiwa ashiriki sehemu ya ile nafaka..sasa mtu huyo endapo akila kile chakula au sehemu ndogo ya kile chake basi anakuwa amekula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.


Na mtu anayekula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu, anakuwa anajiungamanisha na ile madhabahu ya kishetani..ndivyo biblia inavyosema.


1 Wakorintho 10:19-22 “Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?
20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.
22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?


Hiyo ni tahadhari kwetu kuwa tujiepushe na vyakula vya namna hiyo kwani ni hatari kiroho.
Lakini kama umealikwa mahali na umetengewa chakula ambacho kimetolewa sadaka kwa sanamu na ukala bila kujua kuwa kilikuwa kimetolewa sadaka kwa miungu, hapo hupaswi kuogopa kwasababu lile andiko ya kwamba “tutakula vitu vya kufisha navyo havitatudhuru (Marko16:18)” litatimia juu yako.


Lakini kama umeshajua kuwa chakula hicho ni cha miungu basi hupaswi kula kabisa..


Je umewahi kula au kulishwa chakula cha namna hiyo katika familia yenu au ukoo wenu au kwa waganga wa kienyeji?..Kama ndio basi fahamu kuwa siku ulipokula tayari ulijiungamanisha na hiyo miungu, na hivyo roho za hiyo miungu zitayaongoza maisha yako siku zote.


Hivyo suluhisho ili uweze kufunguka ni wewe kwanza kutubu mbele za Bwana kwa kumaanisha na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (Matendo 2:38) na mwisho kupokea Roho Mtakatifu..Kwa hatua hizo utakuwa umefunguliwa moja kwa moja.


Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.

“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

HERI WAPATANISHI, MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments