Jina la YESU KRISTO libarikiwe. Karibu katika kuyatafakari maneno ya Uzima,
Si kila sauti inayokujia kwa faraja, ina lengo la kukupa faraja.. si kila sauti inayokujia kwa kukupa matumaini ina lengo la kukupa matumaini mwisho wake. Hebu tujifunze juu ya Bwana wetu YESU KRISTO, alivyoweza kuzipambanua roho..
Mathayo 16:12 “ Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. 22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. 23 Akageuka, akamwambia Petro, NENDA NYUMA YANGU, Shetani; u kikwazo kwangu; MAANA HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU.”
Mathayo 16:12 “ Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.
22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.
23 Akageuka, akamwambia Petro, NENDA NYUMA YANGU, Shetani; u kikwazo kwangu; MAANA
HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU.”
Nataka tuone hilo neno “MAANA HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU.”.. Kumbe mawazo ya shetani siku zote sio ya mapepo, wala ya mashetani yake bali ya wanadamu!.. Maana yake shetani anaangalia ni nini wanadamu wanakipenda zaidi na kuvitamani na kupitia vitu wanadamu wanavyovipenda na kuvitamani na kuvitafuta ndio vitu hivyo hivyo anatumia kuwaangusha chini katika hatua za mwanzo.
Hapa anajua mwanadamu anapenda “faraja na kutiwa moyo” anakuja kwa gia hiyo hiyo kwa Bwana YESU, akitaka kumfariji kwamba “hatapata mateso, hatakwenda msalabani”.. kwsababu anajua hayo ndio mawazo ya wanadamu siku zote, kutafuta faraja, kutiwa moyo n.k.
Lakini kwasababu YESU KRISTO ni “MWAMBA MGUMU”.. anayajua mawazo ya kila mtu kabla hata hajaambiwa, pale pale alimwona shetani ndani ya Petro, na kumkemea..
Ni kanuni hiyo hiyo shetani anaiendeleza hadi leo, hajabadilika, shetani anayasoma mawazo ya wanadamu wanataka nini na kupenda nini, anajua wanadamu , wanapenda kutiwa moyo, hawapendi kukemewa kemewa, hawapendi kukatishwa tamaa..
Sasa ili baadaye afanikiwe kumkatisha mtu tamaa kikweli kweli, ni lazima aanze kama na kwa kumfariji sasahivi, ili baadaye amvunje moyo kweli kweli, na asiweze kusimama tena, ni lazima aanze sasa hivi kama kwa kumtia moyo..ndicho alichokuwa anataka kujaribu kukifanya kwa Bwana YESU lakini alishindwa.
>Biblia imesema imetupasa “Kuokoka” lakini shetani atakuambia “Bado wakati ngoja kwanza utafute maisha”
>Biblia imesema imetupasa “Kuwa waombaji” lakini shetani atakuambia “wewe upo bize sana, unachoka na kazi”
>Biblia imesema imetupasa “Kuhudhuria kanisani kila jumapili na hata katikati ya wiki (Waebrania 10:25)” lakini shetani atakuambia “kazi zimekuwa nyingi, Mungu atakuelewa tu”.. Ni kama neno la faraja lakini mwisho wake ni huzuni kubwa.
>Biblia imesema imetupasa “Kumtumikia Mungu (Yohana 9:4)” lakini shetani atakuambia “bado wakati, wapo wanaokuombea”
> Biblia imesema imetupasa “kujikana nafsi na kubeba msalaba tunapookoka”.. Lakini shetani atakuambia “usiogope siku moja utajikana tu, ila sasahivi endelea tu kuwa hivo hivo vuguvugu, hakuna mtakatifu duniani”
> Biblia inasema “usiwe mzinzi, na ukizini utakufa” lakini shetani anakuambia hutapata madhara wala hutakufa wapo wanaofanya na wanaishi mpaka leo..
Hayo yote ni mawazo ya shetani ndugu, ambayo ni ya wanadamu!.. Ni lazima tuwe makini katika hili, si kila sauti au wazo linalokuja kwa faraja na matumaini ni la MUNGU, angalia na pima je! Hilo wazo linakubaliana na wazo la MUNGU, kama linakinzana na Neno la MUNGU basi hata kama linakuja kwa sauti ya faraja kiasi gani usisikilize!.. bali sema “NENDA NYUMA YANGU SHETANI KWANI HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU BALI WANADAMU”..
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je wakati Bwana YESU anazaliwa shetani alikuwa amefungwa?
SADAKA INAHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU ZA MASHETANI.
Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?
Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?
Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ