SWALI: Wanafunzi wa Yesu, walimaanisha nini kusema kama “Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa”?
JIBU: Walisema hivyo, baada ya kusikia majibu ya swali lililoulizwa na Mafarisayo kwa Bwana Yesu. Ambapo swali lenyewe lilikuwa linahusiana na talaka katika ndoa, Hivyo wakataka kujua je! Ni sawa mtu kumpa talaka mwanamke kwa sababu yoyote ile mtu anayoiona mbele yake?.
Waliuliza hivyo wakitazamia, majibu ya “Ndio” kutoka kwa Yesu, Lakini kinyume chake, Bwana aliwaambia, Mtu hapaswi kumwacha mke wake, kwa kila sababu anayoiona tu, labda ni mchafu, au mchoyo, au msengenyaji, au hawapendi ndugu zako, au anakudharau, n.k. Hapana, bali sababu tu ambayo aruhusiwa kumwacha mke wake ni ile ya usherati tu, lakini nyingine hakuna..
Mitume waliposikia hayo majibu, ndipo hapo wakamwambia sasa, kama Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.. Ikiwa na maana kuwa kama sababu ni moja tu ya uzinzi? Mbona itahitaji uvumilivu mwingi sana kuiishi hiyo ndoa?.
Embu tusome…
Mathayo 19 :1 Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng’ambo ya Yordani.
2 Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.
3 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe KWA KILA SABABU?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
Maana yake ni kwamba, Mwanamke anaweza akawa sio mzinzi, lakini hana heshima katika nyumba, na tayari kashakuwa mke wako, hapo hauruhusiwi kumwacha, utaendelea naye tu hivyo hivyo mpaka kifo kitakapowatenganisha, Ikiwa mke wako ni mshirikina, na haachi kufanya hivyo vitendo, hupaswi kumwacha na kwenda kuoa mwingine, utaendelea naye hivyo hivyo bila amani mpaka kufa kwako..
Ikiwa mke wako, ni mgumba, hawezi kuzaa, na mmeshaingia katika ndoa, hata kama hatazaa milele utaendelea naye hivyo hivyo bila watoto mpaka kufa kwako..hakuna kutoka nje ya ndoa.
Kanuni hii inatumika pande zote mbili pia hata kwa mwanamke, ikiwa mume wako ulipooana naye alikuwa hanywi pombe, lakini sasa hivi ni mlevi wa kupindukia na ameshindwa kurekebikika, hauruhusiwi kumwacha, utaendelea kuishi naye hivyo hivyo, mpaka kufa kwake,
Kama, alikuwa ni tajiri lakini sasa amefilisika, au kafukuzwa kazi, utaishi naye katika hiyo hali, Kama amepata ajali ni mlemavu, au anamadhaifu Fulani ya kindoa, utaishi naye hivyo hivyo..hakuna talaka
Ndio maana Mitume wakamwambia Bwana, ikiwa mambo ya mtu na mke wake yako hivi ni heri basi mtu aishi bila kuoa, kuepuka hayo yote.
Hivyo Habari hiyo inatufundisha kuwa, kabla ya kuingia katika ndoa tutambue kuwa zipo na changamoto zake nyingi sana,hivyo tuwe tayari kuzibeba, Lakini kama tutaona ni nzito kwetu basi ni heri tubakie kama tulivyo, tusioe wala tusiolewe. Kwani ni vizuri Zaidi, kwa Mungu.
Mithali 21:9 “Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi…
9 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi”.
Fikiri mara mbili,
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)
NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
About the author