Swali: Katika Mwanzo 3:20 na Mwanzo 4:1 mkewe Adamu ni Hawa. Nmekuwa nikisikia mkewe Adamu pia ni Eva. Je! jina Eva na Hawa ni sawa?
Jibu: Hawa na Eva ni jina moja isipokuwa katika lugha mbili tofauti ni sawa na jina YESU na JESUS; ni jina moja isipokuwa katika lugha mbili tofauti, yaani ya kiingereza na ya kiswahili.
Kadhalika na Eva (au Eve) ni kiingereza na HAWA ni kiswahili chake.
Sasa swali ni kwanini, tafsiri zake zionekane kama mbalimbali, yaani Kutoka Eve mpaka Hawa ni kama hazikaribiani?. Kwanini Eve isingetafsiriwa tu Eva kwa lugha ya kiswahili badala yake ikawa Hawa?
Jibu ni kwamba lugha ya kiswahili sehemu nyingi imeitafsiri herufi “V” kwa “W” katika majina ya watu au vitu. Kwamfano utaona jina “LAWI”, kwa lugha ya kiingereza ni “LEVI”.
Vilevile mji wa “Ninawi” kwa lugha ya kiingereza ni “NINEVEH”n.k
Kwahiyo hata Eva kiswahili chake ni lazima kirudi kwenye herufi “w” na kuwa “Hawa”
Ni kama vile majina yote yanayoanza na herufi “J” yanavyobadilika na kuanza na herufi “Y” yanapokuja katika lugha ya kiswahili…Kwamfano Jina Jesus-Yesu, Jonah-Yona, Joshua-Yoshua, Jezebel- Yezebeli n.k Ndivyo ilivyo kwa majina yote yenye herufi “V”, yalibadilika na kuwa “W” yanapoletwa katika lugha ya kiswahili.
Kwahiyo kwa hitimisho mtu anayetumia Jina Hawa na anayetumia Eva wote wapo sahihi, na wanamlenga mtu mmoja.
Je umempokea Yesu?..je umebatizwa?..je umepokea Roho Mtakatifu?..Kama bado unasubiri nini?. Kumbuka hizi ni nyakati za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi.
Maran atha!.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya ELOHIMU?
KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!
Je! dhambi zote ni sawa Kuna dhambi kubwa na ndogo?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)
Rudi nyumbani
Print this post
Amin, thanks.