Tukisoma pale mpaka mwisho inasema;
Marko 2:21 Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; 22 ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kukuu,na pale palipotatuka huzidi. ″Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikukuu;ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. BALI HUTIA DIVAI MPYA KATIKA VIRIBA VIPYA. ??
JIBU: Mfano huo unawalenga watu wote wanaojiona kuwa ni wakristo..Viriba ni vyombo maalumu vilivyokuwa vinatumika zamani kuwekea divai, vilikuwa ninatengenezwa kwa ngozi, sasa nadhani utakuwa unafahamu pombe huwa inafura wakati inapoanza kuchachuka, na pombe zote ndivyo zilivyo, sasa, kwa wayahudi walikuwa wanatumia viriba vya ngozi ambayo bado ni mbichi, hivyo wakiweka divai ambayo bado inaendelea kuchachuka wakati ikiendelea kuvimba basi ile ngozi kwasababu bado ni laini, na mbichi, hutanuka pamoja na divai, kama vile kiatu cha ngozi, unaweza ukanunua mwanzoni kikakubana lakini baadaye utakavyozidi kuendelea kukivaa kinakuenea vizuri kwasababu ni ngozi ambayo haijakakamaa haijawa ngumu bado…
Vivyo hivyo na kwa divai pia,..kwahiyo mfano ile pombe ikiwekwa kwenye kiriba ambacho kimeshakauka au kukaa sana inamaanisha kuwa ile ngozi itakuwa ishakuwa ngumu, kwahiyo ukiweka pombe changa mule ndani ni lazima kipasuke kwasababu ile pombe itavimba na kwa vile hakiwezi kutanuka zaidi mwisho wa siku kitapasuka tu…kwahiyo kiriba kipya, ni kwa divai mpya, huwezi kuweka divai mpya kwenye kiriba cha kale. Hiyo inafunua tabia za wakristo wa leo, ambao roho zao zimegandishwa na mafundisho ya kale, wasiotaka kubadilika kwa kumruhusu Roho wa Mungu kutenda kazi ndani yao, hao ni sawa ni viriba vya kale visivyoweza kutanuka tena, Hivyo mfano ukija ufunuo wa kweli wa Roho Mtakatifu, ufunuo mpya mbele yao ambao hawajawahi kuusikia katika dini zao, au maisha yao, kwasababu ni viriba vya kale visivyotaka kutanuka basi vinapasuka..
Na ndio maana watu kama hao hawawezi kuupokea Ufunuo wa Roho wa Mungu hata kama ni kweli vipi au upo dhahiri kiasi gani, wanaishia kupinga tu kama mafarisayo kwasababu hawana uwezo wa kuchukuliana na ufunuo mpya wa Roho wa Mungu wao wataaishia kupinga tu, na kibakia katika dini zao, na ndivyo walivyokuwa mafarisayo na masadukayo wakati wa Bwana, Yeye alipowaletea kitu kipya hawakuweza kukipokea kwasababu roho zao zilikuwa zimegandishwa na mafundisho yao ya kale. Lakini wale wote waliokubali na kuilainisha mioyo yao kwa Bwana. Basi waliweza kuupokea ndio wale waliokuwa Mitume wa Bwana baadaye. Na ndio maana Bwana akawapa mifano hiyo….
Hivyo ni vizuri kila siku kumruhusu Roho wa Mungu kututengeza kwa jinsi apendavyo ili kuutambua ujumbe wa wakati wako unaoishi…tusije tukawa tunaishi wakati wa ujumbe wa kanisa la kwanza wakati tupo katika ujumbe wa kanisa la mwisho la Laodikia. Kadhalika na mfano wa Kiraka kipya na kikuu kuu maana yake ndiyo hiyo hiyo. Huu ni wakati wa kijiachia mbele za Mungu, mruhusu akufundishe unaposikia jambo jipya ambalo hujawahi kulisikia hapo kabla usikimbilie kupinga tu! Fanya kama watu wa Beroya, lichunguze kwanza kwa maandiko uone kama ni sawa au sio sawa, vinginevyo utakuwa kiriba cha kale, kisichoweza kupokea divai mpya kama wale mafarisayo na Masadukayo.
Ubarikiwe sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada zinazoendana:
ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.
About the author