Azali ni neno linalomaanisha milele, isiyokuwa na mwanzo, wala mwisho.
Hivyo, watu wanaposema Yesu mwana wa Azali wa Mungu, wanamaanisha Yesu mwana Mungu asiyekuwa na mwanzo.
Neno hili utalisikia sana katika, ukiri wa Imani ya Nikea, (kwa makanisa ya kiprotestanti), Imani ya Nikea imetokana na baraza la maaskofu wa kidini waliokaa chini mwaka 325, ili kuunda kanuni moja mama ya imani, ambayo watatembea nayo wakristo wote duniani.
Na huu ndio ukiri wenyewe unavyosema;
“Twamwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Twamwamini Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, Mwana wa Azali wa Baba: yu Mungu kutoka Mungu, yu Nuru kutoka Nuru, yu Mungu kweli kutoka Mungu kweli; Mwana wa Azali asiyeumbwa, mwenye uungu mmoja na Baba: Kwa Yeye huyu vitu vyote viliumbwa. Aliyeshuka kutoka mbinguni kwa ajili yetu wanadamu na kwa wokovu wetu; akatwaa mwili kwa uweza wa Roho Mtakatifu katika Bikira Mariamu, akawa mwanadamu: Akasulibiwa kwaajili yetu zamani za Pontio Pilato; aliteswa, akafa, akazikwa. Siku ya tatu akafufuka kama yanenavyo Maandiko Matakatifu: Akapaa mbinguni; ameketi mkono wa kuume wa Baba: Naye atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu walio hai na wafu. Na ufalme wake hauna mwisho; Twamwamini Roho Mtakatifu Bwana mtoa uzima, atokaye katika Baba na Mwana, anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana, aliyenena kwa vinywa vya manabii; Twaamini Kanisa moja, takatifu, la Kikristo la ulimwengu wote na la kimitume. Twakiri ubatizo mmoja kwa ondoleo la dhambi, Twatazamia kufufuliwa kwa wafu, na uzima wa ulimwengu ujao. Amen”
Je! Ni kweli Kristo ni mwana wa Azali wa Mungu?
Jibu ni ndio. Yeye hana mwanzo wa siku wala mwisho wa Siku. Amefananishwa na Melkizedeki kama maandiko yanavyosema (Waebrania 7:3). Yesu ndio Yehova, na ndio Elohimu katika umbile la kibinadamu. Wala hana tofauti yoyote na Mungu. Ni ofisi tu tofauti za utendaji kazi wa Mungu, lakini ni yeye Yule milele na milele. Wala si Miungu mitatu, katika umoja. Bali ni mmoja katika utendaji kazi wa aina tatu tofauti. Alikuja akakaa kwetu ili kutufundisha namna ambavyo sisi tunavyoweza kuwa wana kamili wa Mungu.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?
Huyu Azazeli ni nani tunayemsoma katika(Walawi 16:8)
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
About the author