Rehani ni nini katika biblia?

Rehani ni nini katika biblia?

Rehani ni nini kibiblia?, na je sisi wakristo tunaruhusiwa kuweka kitu rehani?


Rehani ni mali iliyowekwa kama dhamana kwa mkopo uliochukuliwa, maana yake mkopo usipolipwa basi mali ile inachukuliwa ili kufidia ule mkopo.

Katika biblia (Agano la kale), Rehani iliruhusiwa lakini kwa kuiangalia hali ya mtu. Kama mtu alikuwa ni tajiri mwenye uwezo basi alipokopa alipaswa aweke rehani mali itakayosimama badala ya ule mkopo endapo atashindwa kuulipa.

Lakini kama mtu alikuwa ni maskini sana, na hana kitu isipokuwa jiwe la kusagia tu na mavazi, basi hakupaswa kutozwa rehani katika hivyo alivyo navyo, ilikuwa ni dhambi kubwa kutwaa jiwe la kusagia la maskini au mavazi yake kama Rehani.

Kumbukumbu 28: 6 “Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani”.

Kumbukumbu 24:17 “Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;

18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili”.

Kwa urefu kwanini si sawa kutwaa jiwe la kusagia la maskini kama rehani waweza kufungua hapa >>>Kwanini jiwe la kusagia Mungu alikataza lisiwekwe rehani? (Kumbukumbu 24:6).

Sasa swali je na sisi wakristo ni sahihi kuweka kitu rehani au kupokea rehani kutoka kwa mtu tuliyemkopesha?

Jibu: Rehani haijakatazwa katika biblia, kama umemkopesha mtu kitu cha thamani, na mtu huyo si ndugu yako katika Imani (yaani mpendwa mwenzako) au si ndugu yako katika mwili (yaani mwanafamilia) waweza kupokea Rehani, ili kumhamasisha kurejesha lile deni, (ikiwa lengo lako si kumkandamiza bali kumhamasisha na kama mtu huyo uwezo huo anao). 

Lakini kama ni maskini na kaja kukopa kwako, si vizuri kuchukua rehani. Waweza kumkopa bila rehani yoyote, ni itakuwa baraka kwako.

Lakini kama ni ndugu yako katika Imani na katika damu, si vyema kumtoza rehani,  wala riba, katika mazingira yoyote yale, awe tajiri au maskini,  waweza kumkopa ukitumai kuwa atakulipa tu pasipo kutaka dhamana.

Lakini pia kama wewe ni mkopaji, (maana yake unakopa kutoka kwa mtu/taasisi kwaajili ya shughuli fulani) si dhambi kusimamisha kitu kama rehani itakayosimama kwaajili ya mkopo wako (kama mtu huyo au taasisi hiyo inahitaji hayo yote).

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

“Humfukuza punda wake asiye baba”, nini maana ya mstari huu? (Ayubu 24:3)

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

LIONDOE JIWE.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments