“Humfukuza punda wake asiye baba”, nini maana ya mstari huu? (Ayubu 24:3)

“Humfukuza punda wake asiye baba”, nini maana ya mstari huu? (Ayubu 24:3)

Jibu: Tusome kuanzia ule wa 2 ili tuweze kuelewa vizuri.

Ayubu 24:2 “Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.

3 Humfukuza punda wake asiye baba, Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.”.

Hapa Ayubu anazungumzia juu ya kundi la watu wabaya ambao wanawaonea Mayatima na kuwadhulumu wajane.

Ndio hapo anasema wapo (watu duniani) ambao.

1. Wanaondoa alama za Mipaka, na kuyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.

Maana yake wanawadhulumu watu mashamba/ardhi kwa kuondoa mipaka iliyokuwepo na kuweka mipaka ya uongo!,..na baada ya kumiliki ardhi kwa dhuluma namna hiyo bado wanalisha mifugo yao juu ya hizo ardhi za dhuluma.

2. Humfukuza punda wake asiye baba,

Maana yake humfukuza Punda wa Yatima, (mtoto asiye na Baba). Punda wake anapoingia mahali kula vichache vilivyosalia katika  mashamba yao, wao humfukuza punda Yule, pasipo kuzingatia kuwa Yule ni yatima asiye na uwezo wa kujimudu mwenyewe, asiye na uwezo wa kununulia chakula punda wake, lakini wao hawajali hayo yote, bali wanazifukuza punda zake.

3. Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.

Hawa watu pia wanachukua Ng’ombe za wanawake wajane, ambao wamefiwa na waume zao, na hata nguvu za kufanya kazi tena hawana!.. wanachukua Ng’ombe zao na kuwaweka Rehani, kutokana na mikopo wanawake hao waliyoichukua.. Jambo ambalo ambalo si jema machoni pa Mungu..Wangepaswa wawahurumie na kuwapa mikopo bila kuwawekea rehani chochote kwasababu wao hawana tumaini msaada wowote wapo wao kama wao, na umri wao umeshakwenda..

 Kumbukumbu 24:17 “Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani; 

18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili”

Hivyo watu wa namna hii ambao wanawatesa Wajane na Mayatima, Bwana Mungu alitaja hukumu yao katika kitabu cha Kutoka 22:22

Kutoka 22: 22 “Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.

 23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao, 

24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima”.

Hivyo na sisi hatuna budi kuwatendea Mema watu hawa, na kuwapenda ili na Bwana atubariki

Shalom

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?

Kwanini wajane vijana hawakupaswa kuandikwa?

NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?

TENDA AGIZO LA YESU, HILO NDIO LITAKALOKULINDA.

Nini maana ya “wazimu” katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments