Maana ya Mithali 26:2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,

Maana ya Mithali 26:2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,

SWALI: Nini maana ya Mithali 26:2

Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.


JIBU: Mungu anafananisha laana isiyo na sababu na ndege wanaotanga-tanga angani.

Kama tunavyojua ndege hawa aina ya shomoro na mbayuwayu, kila siku tunawaona wanaruka angani, kila siku tunawaona wapo hari-hari, wanaonekana kama wapo buzy, lakini katika kazi zao zote, na juhudi zao zote, na mikakati yao yote, kamwe huwezi ona yanaleta madhara yoyote kwa mwanadamu. Hata kama utawaharibia viota vyao, hata kama watakauwa na hasira na wewe, huwezi ona wanamshambulia mwanadamu, kwasababu uwezo huo hawana. Huwezi wafikiria na kila wanapokuona wanakimbia. Wewe mwenyewe ukiwaona huwezi kuwaogopa, tofauti na ukimwona nyoka, utajidhatiti asikuume. Lakini ndege huvai ‘chapeo’ kichwani kujilinda naye asikuume, kwasababu hana madhara.

Ndivyo Mungu anavyotufundisha, laana zisizo na sababu, haziwezi kukupata ni kama ndege tu angani, zitapita, na kuendelea na shughuli zake, kamwe haziwezi kukupata ikiwa wewe ni mtakatifu, Hii ni kutufundisha kuwa hatupaswi kuwa waoga wa maneno ya watu  (laana) ambayo hayana sababu.

Ukiona laana imekupata basi  ujue kulikuwa na sababu nyuma yake, (lakini sio tu maneno matupu mtu anayoyatoa), mfano wa laana hizi ni ile ya Elisha aliyowalaani wale vijana 42, walioraruliwa na dubu. Kwasababu walimdhihaki. (2Wafalme 2:22-25)

Lakini mfano wa laana zisizo na sababu, ni ile Goliathi aliyomlaani Daudi kwa miungu yake, ambayo  ilikuwa ni kazi bure..

1Samweli 17:42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri.  43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake

Ni mfano mwingine ni ile Balaamu mchawi alivyojaribu kuwalaani Israeli ikashindakana, kwasababu huwezi laani vilivyobarikiwa. (Hesabu 23)

Hata leo, ikiwa wewe umeokoka, hupaswi kuogopa, maneno yoyote iwe ya waganga au wanadamu. Kwasababu wewe tayari ni mbarikiwa. Ni ajabu sana kuona mkristo,  analia na kutetemeka, eti! Mchawi kamwambia mwaka huu hautaisha atakuwa watoto wake wote watakuwa wamekufa!!. Mzee wa mila kamwambia atapata ajali kwasababu hakutambika kijijini mwaka huu.

Mwingine anawaza, mzazi kamwambia hatafanikiwa kwasababu kaamua kuokoka. Haa! Unaogopa nini hapo?. Hizo ni laana zisizo na sababu. Ishi kwa amani zione tu kama ndege wa angani ambao hukai kuwafikiria kama watakushambulia siku moja.

Ukiokolewa na Kristo umebarikiwa, wewe sio wa kunenewa maneno ovyo ovyo tu, na yakatokea. Wewe ni uzao wa kifalme usiotetemeshwa, ngome imara isiyoangushwa. Mwamba mgumu usiogharikishwa. Yatambue mamlaka na nguvu ulizopewa ndani ya Kristo. Usiogope!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Elewa maana ya Mithali 26:2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,

Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,

Maana yake nini, Mwe na hofu wala msitende dhambi? (Zaburi 4:4)

NUHU WA SASA.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments