USIOGOPE.. USIOGOPE…

USIOGOPE.. USIOGOPE…

Danieli 10:19 “Akasema, Ee mtu upendwaye sana, usiogope; amani na iwe kwako, uwe na nguvu, naam, uwe na nguvu. Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu; kwa maana umenitia nguvu”.

HOFU ni mlango wa Adui, lakini UJASIRI katika Neno la MUNGU ni UFUNGUO wa mafanikio.

Ifuatayo ni mistari michache ya kusimamia wakati wa tufani, na mashaka, na vitisho vya adui na majaribu yake yotw yajapo.. Simama nayo, na utauona Wokovu wa Bwana.

  1. USIOGOPESHWE NA SAUTI YA KIFO.

Waamuzi 6:23 “BWANA akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa”.

2 Samweli 12:13 “Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa”.

  1. USIOGOPSHWE MAJARIBU MAZITO.

Isaya 41:10 “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”.

  1. USIOGOPE KUMTUMIKIA MUNGU.

1 Nyakati 28:20 “Kisha Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Uwe hodari, mwenye moyo mkuu, ukatende hivyo; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu, Mungu wangu, yu pamoja nawe; yeye hatakupungukia wala kukuacha, hata itakapomalizika kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya BWANA”.

Matendo 18:9 “Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze”.

  1. USIOGOPE UNAPOBAKI PEKE YAKO.

Isaya 41:13 “Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia”.

  1. USIOGOPE JUU YA UZAO WA TUMBO LAKO.

Isaya 43:5 “Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi”.

Mwanzo 35:17 “Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine”.

Mwanzo 21:17 “Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko”.

  1. USIOGOPE KUINGIA MJI MWINGINE.

Yoshua 1:9 “Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

Kumbukumbu 1:21 “Tazama, BWANA, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike”.

Mwanzo 46:3 “Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko.

4 Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako”.

  1. USIOGOPE MAJESHI YA ADUI YANAPOJIPANGA.

2 Wafalme 6:16 “Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao”.

Zaburi 27:3 “Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea”.

  1. USIOGOPESHWE NA TAARIFA ZA GHAFLA ZENYE KUHUZUNISHA.

Mithali 3:25 “Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.

26 Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe”.

BWANA AKUBARIKI.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UWE MWAMINIFU HATA KUFA.

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

UWE KIKOMBE SAFI 

UTAJUAJE KAMA WEWE NI MTUMISHI WA MUNGU NA KRISTO YU PAMOJA NAWE?.

Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments