Je unafahamu kuwa “Hukumu ya ibilisi” ilishapitishwa?.. Ni muhimu kulifahamu hili ili tusipumbazwe na dhambi.
Awali turejee maandiko..
Yohana 16:11 “kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa”.
Haya ni maneno aliyoyasema Bwana YESU kuhusiana na hukumu ya ibilisi kwamba imeshapita, na hana wakati tena wa kusimama mbele ya kiti cha hukumu kuhumiwa tena, tayari kashahukumiwa..
Fahamu kuwa kosa kubwa lililomfanya ibilisi kutupwa katika ziwa la moto si kumdanganya mwanadamu, wala hakuna adhabu yoyote anayojiongezea katika kumdanganya mwanadamu… kwanini?, kwasababu tayari alishahukumiwa na hiko ndicho kinachomfanya afanye kazi yake kwa bidii sana ya kudanganya watu na kuwapoteza..
Kosa kubwa ibilisi alilolifanya ni KUASI HUKO MBINGUNI, na akapimiwa kipimo cha adhabu ya juu kikubwa cha kumstahili ambacho ni ZIWA LA MOTO (yenye makali kuliko jua) yeye pamoja na malaika walioasi pamoja naye, kwa ufupi ni kwamba ziwa la moto lilikwisha kuwepo kabla hata ya mwanadamu kuumbwa, kwasababu biblia inatuambia hilo kuwa lilitengenezwa kwaajili ya shetani na malaika zake na si mwanadamu.
Mathayo 25:41 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, ALIOWEKEWA TAYARI IBILISI NA MALAIKA ZAKE”
Umeona?.. moto uliwekwa tayari kwa shetani na malaika zake na si wanadamu, lakini kwasababu wapo wanadamu watakaomfuata ibilisi na kumkataa Mungu, ndipo wataungana na jeshi hilo la ibilisi katika moto huo.
Kwahiyo kamwe tusijidanye kuwa ibilisi ataenda kuulizwa kwanini katupoteza, au kwanini alisababisha wewe uzini, au kwanini alishababisha ajali na watu wakafa, au kwanini aliwatesa watu duniani?..hana hukumu yoyote kwasababu ya kuudanganya ulimwengu, adhabu aliyopewa ni kuasi kule juu, na hiyo adhabu yake ni kubwa sana na ya kutosha..
Siku ile mbele ya kiti cha hukumu ni wanadamu ndio watakaosimamishwa wenyewe kuhukumiwa kwa kadiri ya matendo yao.
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Kwahiyo dada usimlaumu shetani kana kwamba siku ile ataulizwa kwa kukudanganya wewe, yeye hana maswali tena ya kuulizwa, yeye hana hoja tena za kujibu, yeye tayari adhabu yake imeshapitishwa, na hilo ndilo linalomfanya aendelee kufanya uharibifu kwa kasi sana, kwasababu hakuna anachoongeza wala kupunguza katika adhabu yake.
Hata akiua watu elfu kikatili, hakuna kinachoongezeka kwenye adhabu yake kwasababu amekwisha hukumiwa, ule moto ni mkuu sana ibilisi alioandaliwa.
Kwahiyo dada maisha yako ya uchafu yatafakari sana, kaka maisha yako ya uzinzi yatafakari sana, ndugu maisha yako ya uvuguvugu yatafakari sana, usikae umsingizie shetani kana kwamba shetani ataulizwa siku ile kwaajili yako, siku ile utasimama peke yako, nitasimama peke yangu, futa kale kausemi “shetani kanipitia”
Ni heri ukatubu leo na kumpa Yesu maisha yako kabla hizo siku za hatari hazijafika, kabla siku zako za kuishi hazijafika.
Neno la Mungu linasema, mkumbuke muumba wako kabla roho haijamrudia aliyeitoa (yaani Mungu,
Mhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Shetani alitoka wapi?
NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?
Nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.
HIZO NDIZO ROHO ZA MASHETANI.
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ