Shalom, karibu katika kuyatafakari maandiko..
Inafahamika kuwa Kristo alimwaga Damu yake pale Golgotha, pale ambapo misumari ilipopita katikati ya mikono yake na miguu yake, pamoja na mapigo mengine mwili mzima. Kwa damu ile iliyomawagika tulipata ondoleo la dhambi na ukombozi wa Roho zetu,
Lakini Damu hiyo hiyo, tunasoma haikuanza kumwagika saa hiyo ya Mateso ya msalaba…Bali ilitangulia kumwagwa wakati Bwana akiwa anaomba pale kwenye mlima wa Mizeituni pamoja na wanafunzi wake,
Sasa ilimwagika kwa jinsi gani?.. si kwa jinsi nyingine bali kwa jinsi ya JASHO LAKE
Luka 22:44 “Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; HARI YAKE IKAWA KAMA MATONE YA DAMU YAKIDONDOKA NCHINI.]”
Sasa swali la msingi ni kwanini, itoke wakati akiwa katika MAOMBI?.. Ni kwasababu maneno pekee hayatoshi kufikisha maombi kwa Baba, bali Damu inanena zaidi kuliko maneno, na Hivyo ile damu iliyokuwa inamwagika wakati wa maombi ilinena zaidi kuliko maneno tu.. Kwa namna gani tunalithibitisha hilo??..Turejee habari ya Habili.
Biblia inasema Damu ya Habili ilinena ardhini baada ya kuuawa kwake..ijapokuwa alikufa lakini ile damu ililia na kuomboleza mbele za Mungu.. (soma Mwanzo 4:10) na Mungu akaisikia, na ikaleta kisasi kwa Kaini aliyemwua..
Vile vile maombi ya Bwana YESU pamoja na Damu yake inayomwagika ardhini kabla ya mateso ya msalaba.. ilinena zaidi na ndio maana baada ya pale, walitumwa Malaika kumtia Nguvu..na tena Damu ya YESU inanena mema kuliko ile ya Habili..
Waebrania 12:24 “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili”.
Na wakati huu tunapoomba kwa kufahamu Ufunuo huo uliopo katika Damu ya YESU, tutapenda MAOMBI!.. tukijua na kuamini kuwa ipo damu ya YESU inayochuruzika sasa kwaajili yetu tunapoomba.. na hiyo damu inanena mema zaidi ya maneno yetu.
Lakini kama tupo nje ya Imani ya kumwamini Bwana YESU KRISTO, damu yake hiyo haiwezi kunena mema kwaajili yetu, ili iweze kunena mema na kumshinda Yule Mwovu, na hata kuvuta majibu ya maombi, ni sharti kwanza kumwamini Bwana YESU na kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha na kubatizwa ubatizo wa maji na Roho, kuanzia huo wakati na kuendelea ile damu inakuwa inanena mema kwaajili yako na utakuwa unazo nguvu za kumshinda shetani.
Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
NA SISI TUTOKE TUMWENDEE NJE YA KAMBI.
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.
Konstantino mkuu ni nani, na je anaumuhimu wowote katika ukristo?
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ