NA SISI TUTOKE TUMWENDEE NJE YA KAMBI.

NA SISI TUTOKE TUMWENDEE NJE YA KAMBI.

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Katika agano la kale ilikuwa ni sheria, ili sadaka ya upatanisho, au ya dhambi ambayo ilihusisha kafara za wanyama, kuwa kamili, ni lazima uhusishwe na sehemu kuu mbili, ya kwanza ni ndani ya kambi, na ya pili ni nje ya kambi.

Ndani ya kambi au ndani ya lango, ndio ilichukuliwa damu ya mnyama huyo na kuingizwa kwa ajili ya upatanisho kwa kunyunyizwa. Lakini ilikuwa ni sharti pia viungo, ngozi na vinyesi, vya mnyama huyo vikateketezwe mbali nje ya kambi. Na kama jambo hilo lisipofanyika, haijalishi damu ya kunyunyiza ya mnyama  huyo itakuwa ni njema kiasi gani, utapatanisho hauwezi kutokea.

Ndani ya kambi ni mahali patakatifu, lakini je! Ya kambi ni mahali pa uovu.

Sasa tukirudi kwenye agano jipya, tunaona mwokozi wetu Yesu Kristo, anafananisha na mnyawa huyo wa upatanisho, Hivyo ilimbidi, ahusishwe pia na sehemu zote mbili, yaani ndani ya kambi na nje ya kambi.

Alimwaga damu yake, ambayo kwa kupitia hiyo, ameingia nayo  patakatifu pa patakatifu kule mbinguni, kutuombea sisi, Lakini hilo lisingewezekana, kama asingeteketezwa nje ya kambi.

Ndio Hapo tunaona Bwana wetu, ilimpasa, aache enzi na mamlaka mbinguni, (Atoke nje ya kambi), akutane na waovu huku duniani, ateketezwe kabisa mahali pa aibu pa waovu pale Golgota, ili sasa damu yake ipatikane kufanya upatanisho wetu kule mbinguni, kwa Baba ambapo ndio ndani ya kambi.

Na matokeo yake ndio haya tunayoyaona sasa hivi, sote kupata neema na ondoleo la dhambi zetu.

Lakini sasa maandiko yanasema..

Waebrania 13:11  Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi.

12  KWA AJILI HII YESU NAYE, ILI AWATAKASE WATU KWA DAMU YAKE MWENYEWE, ALITESWA NJE YA LANGO.

13  BASI NA TUTOKE TUMWENDEE NJE YA KAMBI, TUKICHUKUA SHUTUMU LAKE.

14  Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

Umeona hapo? Kumbe na sisi, hatuna budi kumfuata Yesu nyayo zake, kwasababu alisema mimi nilipo na mtumishi wangu atakuwepo.  Sasa hapo anasema, na sisi tutoke nje ya kambi, tuchukue shutumu lake. Akiwa na maana, tukubali kujitoa sadaka na sisi, nje ya lango, waovu walipo ili tuwavute wengine kwa mwokozi.

Kama mashahidi  wa kweli wa Kristo, ni lazima tuwe tayari kuhatarisha maisha yetu, kwa ajili ya wengine. Tusiwe tu ndani ya lango, walipo watakatifu, ni kweli ni vizuri kufanya semina za ndani makanisani zina nafasi yake, ni vizuri kuhubiri mikutano ya ndani. Lakini je! Tunaweza tukawa tayari pia kwenda katikati ya watu wa dini nyingine kuwahubiria Kristo, tukawa tayari kwenda mahali pa jamii zenye vita na kuzitangaza habari za Yesu. Kanisa la Kwanza la mitume lilikuwa tayari kutoka nje ya kambi, kukutana na ukinzani wa wayahudi, kuburutwa, kupigwa mawe hata kuawa, walikuwa tayari kuwaendea wapagani sugu, na jamii za wachawi kuwatangazia Kristo. Vivyo hivyo na sisi hatuna budi kutoka nje ya kambi, kuliendea na kundi lingine ambalo halijamjua Kristo.

Hatuna budi kuwa tayari hata kuhatarisha afya zetu, fedha zetu, kazi zetu,  vyeo vyetu, elimu zetu inapobidi ili wengine waokoke, wamjue Kristo. Huko ndiko kutoka nje ya kambi. Bwana Yesu ilimpasa aache enzi na mamlaka juu mbinguni, awaendee makahaba na watoza ushuru, awaendee waliosumbuliwa na ibilisi na mapepo, na sio kwa makuhani na waandishi, ijapokuwa na hao pia alikuja kuwafia, lakini nguvu zake nyingi zilikuwa kwa wenye dhambi.

Bwana atupe neema hiyo.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

UWEZA WA MUNGU NJE YA WAKATI.

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

USIWE ADUI WA BWANA

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments