JIBU: Ili kupata jibu ya swali hilo, ni vizuri pia tujiulize baadhi ya maswali ambayo ni rahisi kabisa kuyajibu yanayoonekana katika maisha yetu ya kila siku. Tuchukulie mfano Leo hii nikimuuliza daktari je! Utanithibitishiaje kuwa kama kuna kitu kinachoitwa kirusi au bacteria.?..
Tunafahamu hataniita na kuniambia angali kwa makini utaviona hewani , vikielea, vinginevyo nitamuona ni mwendawazimu lakini yeye kama daktari atajua kabisa kwa macho yangu ya asili siwezi kuviona virusi au bacteria hivyo jambo yeye atakalolifanya ni moja kwa moja kunichukua na kunipeleka mahabara na kunionyesha KIFAA maalumu kinachoitwa HADUBINI (Microscope), ambacho hicho kimeundwa mahususi kwa ajili ya kuvuta vitu visivyoonekana kwa macho. Hivyo pale nitakapoitazama labda tusema damu kwenye hadubini hiyo na kuona vijidudu vidogo vidogo vikitembea ndipo hapo nitakapoamini kuwa kuna viumbe vinaitwa Bacteria au virusi.
Kadhalika leo hii mtaalamu wa masuala ya Anga, akaniambia kuna sayari inayoitwa Pluto inayofanana na dunia, ni wazi kuwa siwezi kuamini kwasababu kwa macho yangu hayalithibitishi hilo lakini pindi atakapotumia kifaa chake maalumu kinachoitwa DARUBINI (Telescope). Ambacho hicho ni mahususi kwa kuvuta magimba yote yaliyo angani ndipo nitakapoamini kuwa kweli kuna sayari inayoitwa Pluto kwasababu ninaiona kwenye darubini. Vivyo hivyo na mambo ya rohoni, hatuwezi kuyatambua kwa jinsi ya mwilini biblia inatuambia hivyo katika
1Wakoritho 2: 14 “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni”.
Hivyo ili sasa tuweze kujua kuwa kuna mbingu au kuzimu basi yatupasa nasi pia tutumie kifaa maalumu kinachoweza kuvuta mambo ya rohoni na hicho si kingine zaidi ya BIBLIA TAKATIFU. Tatizo linakuja ni pale watu wasipotaka kuliamini NENO LA MUNGU na huku bado wanataka wamwone Mungu, ni sawa na mtu anayetaka kuona kirusi na huku bado haiamini Hadubini. Iamini kwanza biblia, ndipo utakapopata uthibitisho kweli kama kuna mbingu au kuzimu vinginevyo hata mtu atoke mbinguni au kuzimu akuambie hutaamini wala hutaweza kulithibitisha hilo.
Ubarikiwe sana.
Mada zinazoendana:
KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI ,JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?
JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?
NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.
NJIA YA MSALABA
MAFUNDISHO YA MASHETANI
NGUVU YA MUNGU YA UUMBAJI
Rudi Nyumbani:
Print this post
Nawapongeza, kwa mafundisho yenu mbarikiwe na Mungu azidi kuwafunulia zaidi
Amina, Patrick, ubarikiwe nawe pia na Bwana akuongezee Neema yake.