Amani ya Bwana Ni nguzo ya Muhimu sana katika kumwongoza Mkristo.
Moja ya njia Mungu anazotumia kuzungumza na Mtu ni kwa kupitia amani…
Vivyo hivyo na Mungu wetu anazungumza na sisi mara nyingi kwa kupitia AMANI.
Akitaka kukuzuilia jambo fulani lililo nje ya mapenzi yake, utaona umekosa amani ghafla ya kufanya jambo hilo.
Hata katika maombi..moja ya uthibitisho kama maombi yako yamejibiwa ni AMANI UTAKAYOIPATA; Kama moyo wako umekuwa mzito, pengine una majonzi, huzuni, umekosa furaha na unatamani Mungu azungumze na wewe, ingia kwenye magoti omba mpaka uone amani fulani imeingia ndani yako..Ukiona kuna amani imekuja ndani yako ya kipeee Hapo jua Roho Mtakatifu katenda jambo.
Na amani hii inapokuja juu yako utaona inakufanya unazidi kumpenda Mungu zaidi, na utaona inakusukuma kutenda wema zaidi kuliko ubaya…utajikuta kama kuna mtu au kitu kilikuwa kimekuudhi ghafla unaona unahaja ya kusamehe, ghafla unasikia kama vifungo fulani vimeachia…ulikuwa unampango wa kulipiza unajikuta unasamehe, ulikuwa na hasira ghafla unajikuta furaha fulani imekuvaa..kadhalika uchangamfu fulani unakuingia..n.k hiyo ndiyo amani ya Kristo..Amani ya ulimwengu huu, matunda yake ni kutenda dhambi…ulikuwa na hasira na ulipofikiria kwenda kulipiza kisasi amani fulani ikakuingia kwenda kufanya hicho kitendo hiyo ni amani ya ulimwengu huu..
Bwana Yesu alisema katika kitabu cha Yohana..
Yohana 14:27 “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.
Ni muhimu kuitafuta sana Amani ya Kristo.
Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”
Wakolosai 3:14 “Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. 15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani”.
Hii Amani ya Mungu chanzo chake ni KUOKOKA! na mtu unaokoka kwa kutubu kwanza na kudhamiria kuacha dhambi zako na kisha kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu.
Itafute Amani ya Mungu, ambayo ndio amani ya moyo inayolenga mapenzi ya Mungu. kwasababu inapatikana…kumbuka alisema mwenyewe kuwa “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo.”
Ubarikiwe.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
NYOTA ZIPOTEAZO.
KUONGEZEKA KWA MAARIFA.
UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUZAA MATUNDA.
MAFUMBO YA MUNGU.
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA
Rudi Nyumbani:
Print this post