Mhubiri anasema… “Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili”(Mhubiri 11:8 ).
9 Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni..”
Huyu ni Sulemani ambaye tunamjua alikuwa ni Mfalme mwenye hekima. Na bado ni Tajiri ambaye hakuonekana mfano wake katika historia, alipitia utoto kama vile wewe ulivyo mtoto leo, alipitia ujana kama vile wewe ulivyo kijana leo. Alipitia pia uzee kama vile wewe ulivyo mzee leo, na kila hatua aliliandikia hekima yake inayomfaa mtu husika. Lakini leo hii tutaangalia kipengele kimuhusucho kijana, anasema kama wewe ni kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako. ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni..
Mungu kakupa uzuri, Mungu kakupa urembo, Mungu kakupa afya njema, Mungu kakupa elimu nzuri, Mungu kakupa kipaji kizuri, Mungu kakupa hata utajiri, vyote hivyo ni vyema kuwa navyo, uvifurahie na kuviishi…Unafanya vyema kuwa na malengo mazuri, kuwa na biashara nzuri, kuwa na kampuni zuri, kuwa na mke mzuri,..lakini fahamu kuwa katika hayo hayo unayoyafikiria na kuyatenda sasa, huku huku ndiko Mungu atakapokuhukumia..
Ikiwa wewe katika ujana wako unaona ni vema uvae nusu uchi ukazunguke barabarani watu wote waoune uchi wako. Na umbile lako kisa tu wewe ni unajiona ni mrembo basi fahamu kwa ajili ya hayo Mungu atakuleta hukumuni..Ikiwa unafanya biashara na pesa yako inakujia kwa njia ya kuhonga basi ujue kuwa kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni. Ikiwa umemwona mke wa mtu, ukampenda ukamchukua ukaishi naye mkazaa naye mkawa na Maisha mazuri ya furaha yasiyo na masumbufu basi ufahamu kuwa ajili ya hayo unayoyafanya Mungu atakuleta hukumuni…Ikiwa leo hii unajionyesha kwamba wewe ni kijana wa kisasa, unakunywa pombe, unavuta sigara,. Unahudhuria disko, na unaona hakuna shida yoyote kufanya hivyo, ni mambo tu ya ujanani,
Jambo lolote lile leo hii unalolifanya au,unalojishughulisha nalo basi tarajia kuwa siku ile ikifika hicho hicho ndicho kitakachokupeleka hukumuni..Mungu hawezi kukuleta hukumuni kwa mambo usiyoyajua, au usiyoyafanya, au usiyoyafikiria, haiwezekana ukawa ni muuzaji wa madawa ya kulevya siku ile ukaenda kukuuliza habari za kwanini ulikuwa fisadi., hapana, palepale kwenye malengo yako, palepale kwenye shughuli yako hapo hapo ndipo patakapozungumza katika siku ile..
Na ndio maana mhubiri anatushauri na kusema.. Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi…
Tunapopewa Maisha marefu, tunapoona tunafanikiwa katika jambo lolote lile, liwe ni baya au ni jema, basi tufahamu kuwa pia zipo siku za giza zinazokuja huko mbeleni. Ambazo nazo zitakuwa ni nyingi hata Zaidi ya hizi tunazoziishi, wakati ambayo kitabu cha kila mmoja kitafunguliwa, na kusomwa aya baada ya aya. kurasa baada ya kurasa, siku baada ya siku ya Maisha yako aliyokuwa anaishi hapa duniani…Hapo ndipo tutahukumiwa sawasawa na kile kitabu cha uzima.
Hivyo Mhubiri anatuonya tuyachunge Maisha yetu katika hizi spidi za Maisha tulizonazo, tuumie ujana wetu vizuri, kama wewe ni kijana, sio kila fashion inayokuja uikimbilie, sio kila fursa ya biashara inayokuja mbele yetu tunaichangamkia kisa tu inapesa, tuipime je itatukosesha na Mungu au la?.
Kwasababu kwa kupitia hiyo ndio tutahukumiwa. Sio kila mwanamke au mwanamume anayekuja mbele yetu ni wa kuoa au kuolewa kisa tu anayo fedha au ni mzuri, tuangalie je! Anakidhi vigezo vya Ukristo?. Je alishaoa au kuolewa kabla ya kukutana na wewe?. Tusije tukahukumiwa kwa dhambi za watu wengine. Kwa maana ukiolewa au ukioana na mtu ambaye amemwacha mke/mume wake ni unazini. Na wazinzi wote sehemu yao ni katika lile ziwa la moto, Biblia inasema hivyo.
Sio kila Rafiki ni wa kuongozana naye tuangalie je! Ni mtukanaji?. Ni mzinzi, ni mwizi n.k., tusije tukajifunza tabia zake takajikuta na sisi tunahukumiwa kwa ajili yao..Kwasababu yote tunayoyafanya, yanayotuzunguza ndio hayo tutakayo hukumiwa nayo. Ni heri tukakosa vingi lakini siku ile tuwe upande salama, kuliko kupata vyote na kujikuta katika ziwa la moto.
Mhubiri 4: 6 “Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo”.
Ikiwa bado hujaokoka, Na unahitaji kumpa Bwana Maisha yako leo ayasafishe kwa damu yake. Na ayaongoze, awe mtetezi wako hata siku ile ya hukumu. Utakuwa umefanya jambo jema na la busara ambalo hutakaa ulijutie milele..Unachotakiwa kufanya hapo ulipo, ni ujitenge kwa muda kidogo peke yako.
Kisha piga magoti kuonyesha utiifu wako kwa Mungu na kwamba unahitaji msaada wake. Kisha hatua inayofuata ni kumweleza Mungu kwa kumaanisha kabisa kuwa umetubu dhambi zako zote leo. Na kwamba kuanzia sasa unataka umwishie yeye hadi siku ile utakapokwenda mbinguni…
Hakikisha unatubu kwa kumaanisha kabisa. Kwasababu toba halisi sio kuongozwa sala fulani kama inavyodhaniwa na watu wengi. Toba halisi ni kutoka moyoni, na Mungu akiona umemaanisha basi hapo hapo anakusamehe pasipo masharti…
Hivyo ukishatubu hatua inayofuata ni kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamwishwa katika maji mengi kwa Jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38, kama bado hujabatizwa. Na baada ya hapo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu kukusaidia na kukulinda mpaka siku ile ya ukombozi wa mwisho wa miili yetu.
Hivyo zingatia hatua hizo ili na wewe ufanyike kuwa mwana wa Mungu, mwenye kustahili kuuridhi uzima wa milele. Na hivyo siku ile ya hukumu mbawa za Kristo zitakufunika kwasababu umehesabiwa haki bure kwa neema yake kwa kumwamini tu yeye.
Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
About the author