Uzao wa Mwanamke ni upi? Unaozungumziwa katika Mwanzo 3:15?

Uzao wa Mwanamke ni upi? Unaozungumziwa katika Mwanzo 3:15?

JIBU: Uzao wa Mwanamke ni Uzao wa Yesu Kristo. Wote waliozaliwa mara ya pili, kwa lugha nyingine ya rohoni wanajulikana kama “uzao wa mwanamke”. Sasa ni kwasababu gani wanaitwa hivyo?.

Tukirudi Pale Edeni tunafahamu kuwa mwanadamu wa Kwanza kuumbwa alikuwa ni Adamu. Watu wote tuliopo sasa wakike na wakiume asili yetu ni kutoka kwa huyu mtu mmoja Adamu!. Ambaye anajulikana kama Adamu wa Kwanza. Alikuwa hana Baba wala Mama. Aliumbwa kwa viganja vya Mungu mwenyewe.

Lakini Adamu wa pili hakuumbwa kutoka katika mavumbi ya ardhi kama Adamu wa kwanza. Bali alizaliwa kutoka katika tumbo la Mwanamke. Na huyo si mwingine zaidi ya Yesu Kristo mwokozi wetu. (1Wakorintho 15:45) ambaye alizaliwa kutoka katika Tumbo la mwanamke anayeitwa Mariamu. Hana Baba wa kimwili ndio maana hajaitwa ni uzao wa mwanamume bali wa mwanamke. Ndivyo ilivyompendeza Mungu iwe hivyo! Hakumhusisha mwanamume katika Kumleta Kristo bali alimhusisha mwanamke peke yake!. Kwasasa ile damu safi itakayowaokoa wanadamu isiyo na mawaa, ilipaswa itoke juu, kwa Mungu mwenyewe..

Sasa Bwana Yesu kuzaliwa na Mwanamke Mariamu hakumfanyi, Mariamu au mwanamke mwingine yeyote kuwa wa kipekee sana kuliko watu wengine, na hata kufikia kiwango cha kuhusishwa na mambo ya ibada kama Kanisa Katoliki linavyofanya. Hapana! Mariamu ametumika kama njia tu..Lakini hakuna la ziada hapo, baada ya kumzaa Yesu alihitaji wokovu tu kama wanawake wengine, alihitaji kumwamini, kutubu na ubatizwa na kuishi maisha matakatifu na ya uangalifu kama watu wengine tu.

Ni sawa na Daudi alivyotumika kama njia ya cheo cha ufalme wa Kristo. Lakini hakukumfanya Daudi kuwa mtu wa kipekee sana kuliko wengine. Kwasababu Yesu mahali pengine anajulikana kama MWANA WA DAUDI! Maandiko yanasema hivyo sehemu nyingi na yeye mwenyewe Yesu alisema yeye ni mzao wa Daudi katika Ufunuo .

Tunasoma katika..

Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi”.

Lakini sehemu nyingine pia anasema Daudi alimuita yeye Bwana, sasa iweje yeye awe tena Mwana wake tena.

Mathayo 22:41 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?

42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.

43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,

44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?

45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?

Au Sasa Tuanze kuweka sanamu za Daudi na kumwomba atuombee na kumwambia salamu Daudi Baba wa Yesu tuombee huko uliko??..Unaona haiingii akilini hata kwa mtoto mchanga wa kiroho anayejifunza biblia kwa mara ya kwanza leo? kama hatuwezi kufanya hivyo kwa Daudi hatupaswi pia kufanya hivyo kwa Mariamu wala mtu mwingine yeyote. Hao wote wametumika kama njia tu ya kupitishia kusudi la Mungu.

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

YONA: Mlango wa 2

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

JE YESU ATARUDI TENA?

JE NI KWELI BWANA YESU SIKU YA KURUDI ATAFIKIA ISRAEL

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments