Jambo moja linalowachanga watu wengi wa Mungu, ni kutokujua Ujio wa Yesu utakuwaje.
Ujio wa Bwana Yesu umegawanyika katika sehemu kuu 3. nazo ni UJIO WA KWANZA, UJIO WA PILI na UJIO WA TATU.
UJIO WA KWANZA: Ni wakati Bwana Yesu alipozaliwa na Bikira Mariamu, na kuifanya kazi yake kwa miaka mitatu na nusu, na kufa, na kufufuka, kisha kurudi mbinguni alikotoka. Huo ulikuwa ni ujio wa kwanza.
UJIO WA PILI: Utakuwa ni wakati wa unyakuo…Ujio huu hautahusisha Bwana kushuka kabisa duniani, bali Bwana atakuja na ataishia mawinguni, sisi tulio hai tutaungana pamoja na wale waliokufa katika Kristo, kwa pamoja tutanyakuliwa kwenda kumlaki mawinguni, na kwenda mbinguni kwenye karamu yake aliyotuandalia, (1 Wathesalonike 4) ambapo huko tutakaa kwa muda wa miaka 7…
UJIO WA TATU: Utahusisha Bwana kurudi tena na watakatifu wake duniani walionyakuliwa, atakuja duniani kwa ajili ya Hukumu ya Mataifa, Vita ya Harmagedon, pamoja na kuanzisha utawala mpya duniani wa Amani utakaodumu kwa miaka 1000. Ujio huu ndio kila jicho litamwona akija wa majeshi ya mbinguni..Na atashukia Israeli. Hapo ndio yatakuwa makao yake makuu kipindi cha utawala wake duniani.
Kwa urefu wa ujio huo pitia somo hapa chini linalosema UTAWALA WA MIAKA 1000.
Mada Nyinginezo:
NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE
About the author