SALA YA ASUBUHI

SALA YA ASUBUHI

Sala ya Asubuhi inapaswa iweje?..Na je kuna sala ya jioni pia?

Hakuna sala rasmi ya Asubuhi iliyotungwa kwamba watu wafuate mfumo wake lakini ni wajibu wa kila mtu anayeitwa mkristo kusali..Katika kusali au kuomba kuna vitu vikuu vitatu vya kuzingatia katika sala yoyote ile.. Cha kwanza ni Shukrani, cha pili ni kupeleka mahitaji na cha tatu ni kutangaza

Katika sala ya Asubuni pia ni muhimu kuzingatia hivyo vipengele vitatu. Mwishoni somo hili kuna somo lingine lenye kichwa kinachosema “FAIDA ZA MAOMBI”. Nakushauri ulisome ili uweze kuelewa uchambuzi wa vipengele hivyo vitatu vya maombi.

Lakini kama ndio kwanza umempa Kristo maisha, basi sala hii hapa chini kwa Asubuhi inaweza kukufaa. 

Unapoamka kabla ya kufanya kitu chochote kile, hata kabla ya kwenda kupiga mswaki.. Sali sala hii kwa kumaanisha na kwa muda mrefu kwa jinsi uwezavyo ukitaja hata  mambo ambao hayajaandikwa katika sala hii.

Sema…

Ee Baba yangu, Mungu muumba wa mbingu na nchi, nakushukuru kwa kuniamsha nikiwa mzima wa afya,(hata kama umeamka na udhaifu fulani mdogo huna buni kumshukuru Mungu pia)

Nasema ahsante sana ni kwa Neema zako tu, wapo ambao hawajaweza kuamka leo lakini mimi nimeamka.

Nakuomba unipe Neema yako katika siku ya leo inayoanza nikatembee katika mapenzi yako, nisikutende dhambi wala nisikuhuzunishe kwa jambo lolote, naomba ukaniepushe na majaribu yote, na mipango yote mibaya ya yule Adui aliyoipanga juu yangu na juu ya watu wangu na vitu vyangu na afya yangu na shughuli zangu katika hii siku ya leo.

Nijalie pia siku hii ya leo angalau niongeze kitu kimoja katika ufalme wako, hata itakapofika tena jioni nikapate kushuhudia matendo yako makuu na kukushukuru. Naomba haya machache katika Jina la Yesu Kristo.

Amen’.

Kumbuka pia tuna wajibu wa kusali muda wote na mahali popote sio tu asubuhi, au jioni…hapana bali hata tukiwa tunatembea, tunafanya kazi..tuna wajibu wa kuomba…sala ya jioni pia ni ya muhimu sana kama tu ilivyo sala ya Asubuhi.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

FAIDA ZA MAOMBI.

FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU

UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.

KIFO CHA MTAKATIFU POLIKAPI (Policarp).

HERI NINYI MLIAO SASA, KWA SABABU MTACHEKA.

JE NI KWELI MTU ANAWEZA KUTOKA NJE YA MWILI WAKE?.

MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
13 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Wasike Amos
Wasike Amos
1 year ago

Amina na jina la Bwana Yesu Kristo litukuzwe….

joshua
joshua
1 year ago

jina labwana litukuzwe

Anonymous
Anonymous
2 years ago

amen jin la bwana litukuswe

J korir
J korir
2 years ago

Amen jina bwana litukuzwe

Ezra Tossi
Ezra Tossi
3 years ago

Asant sana kwa kupata tovuti hii itanifundisha kila kitu

Sila
Sila
3 years ago

Barikiwa sana mtumishi

Kunze
Kunze
3 years ago

Asante. Tuendelee kutiana nguvu ili kuifikia toba.pata email yangu,tuendelee mapambano dhidi ya adui shetani

Henry Nyakundi Mwamba
Henry Nyakundi Mwamba
3 years ago

Nimeshukuru sana, nimepata kusoma na kujifunza jinzi ya kuomba, pata email address yangu uendelee kunitia ngufu kiri.Asanteni