KUOTA UNATEMBEA JUU YA MAJI.

KUOTA UNATEMBEA JUU YA MAJI.

Nini maana ya Kuota unatembea juu ya maji ?.


Kama tunavyojua stori ya mtu mmoja  katika biblia ambaye alirekodiwa kutembea juu ya maji, ni Bwana wetu Yesu Kristo peke yake.

Lakini swali la kujiuliza, ni kwanini aamue kufanya vile? Kulikuwa na umuhiimu gani wa yeye usiku  ule kutembea juu ya maji? Je, ni kwasababu alikuwa anawahi mahali fulani, au alikuwa anawaonyesha tu wanafunzi wake ukuu wake..

Tunafahamu kuwa kila jambo alilolifanya Bwana Yesu, lilikuwa na somo la kutufundisha sisi, na wala sio kutuburudisha..Hata kitendo cha kupaa kwake tu, kilibeba ujumbe mzito kwetu sisi.

Ukifahamu hilo utajua pia sababu ya kwanini wewe unaota ndoto za mara kwa mara unatembea juu ya maji.

Sasa kabla Bwana Yesu usiku ule kutembea juu ya maji utaona alitumia masaa mengi sana kule mlimani katika kusali, hakutembea kwanza bila kuwepo uweponi mwa Bwana muda mrefu..ndipo baadaye sana, akaondoka kuwafuata wanafunzi wake mle baharini, na  alipoikaribia boti walimwona kwa mbali wakaogopa lakini Petro akajitia ujasiri akaomba amfuate kule alipo. Bwana hakumkatalia, akamwambia Njoo, ndipo Petro akaanza kutembea, akapiga hatua kadhaa, akadhani ni rahisi kama anavyofikiria, Lakini wimbi lilipomjia akaogopa akaanza kuzama..

Lakini Bwana Yesu alimwambiaje?, Embu Tusome..

Mathayo 14:25  “Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.

26  Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.

27  Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.

28  Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.

29  Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

30  Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

31  Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka”?

Sasa kama ukiitafakari hiyo Habari kwa karibu utagundua somo Kristo alilokuwa anawafundisha wanafunzi wake, ni kuwa YOTE YAWEZEKANA KWA MTU ASIYEKUWA NA SHAKA..

Lakini sasa hayo mashaka mtu anayaondoaje..ndipo baadaye alikuja kuwaambia wanafunzi wake.. jinsi ya kuondoa shaka rohoni..

Mathayo17:21  [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.

Na ndio maana kabla ya tukio lile Bwana alikuwa katika sala muda mrefu..

Hivyo uotapo ndoto za wewe unatembea juu ya maji, au unakimbia juu ya maji au unapaa wakati mwingine.. Ujue ni Mungu anakukumbusha Habari ile ya Kristo kuwa yote yanawezekana..Lakini haiwezekani kirahisi rahisi tu bali kwa kufunga na kuomba (yaani kwa  kujiweka karibu na Mungu kwa wakati mwingi uwezavyo.)

Sasa ikiwa wewe ni mwenye dhambi, hakuna lolote litakalowezekana kwako lile ambalo haliwezekani kibinadamu..Ikiwa Kristo yupo mbali na wewe (yaani hujamkabidhi Maisha yako)..Huwezi kufanya kila kitu..

Vilevile ikiwa umeokoka, na huna muda Mungu, yaani hata huwezi kujitengea muda kusali hata lisaa limoja kwa siku, husomi Neno, huna bidii ya kuishi maishi yampendezayo Mungu,..kamwe huwezi kutenda yale yasiyowezekana kwa macho ya kibinadamu.

Hivyo kama hujaokoka, ujumbe huu ni wako, mkaribishe Yesu maishani mwako leo..Hapo ulipo dhamiria kwanza kuacha mienendo yako yote ya dhambi, kisha ndio uje uombe rehema Mungu akusamehe, kama hujadhamiria basi ni heri usimwombe Mungu msamaha, kwasababu utakuwa unamdhihaki..Geuka kivitendo, ndipo umwomba Mungu rehema na yeye atakusamehe,..

Uthibitisho kuwa amekusamehe, ni ile amani atakayoileta ndani yako..Na kuanzia hapo anza kuishi maisha ya kikristo..nenda kabatizwe ikiwa hujafanya hivyo, na Roho Mtakatifu atakuja juu yako kukusaidia kutimiliza yale ambayo yatakuwa yamesalia.

Vilevile ikiwa wewe ulikuwa tayari ndani ya Kristo lakini ulizembea zembea wakati wako ndio huu wa kuyatengeneza upya, ukizingatia hizi ni nyakati za mwisho..ongeza viwango vyako vya maombi, funga, jifunze biblia sana, kuliko kitu kingine uwezacho kujifunza, pia ongeza viwango vyako vya Maisha ya utakatifu..Na wewe mwenyewe utaona jinsi utakavyoweza kufanya visivyowezekanika kirahisi sana.

Mambo ambayo kwa namna ya kawaida yaliyonekana hayawezaniki kwa mtu kama wewe kuyafanya lakini ukiitii hiyo kanuni ya Kristo hapo ndipo watu watakaposhanga kukuona ukifanya..ndio tafsiri ya ndoto yako..lakini kumbuka tena neno hili..

 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga. (Mathayo17:21) shalom.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?

KUOTA MAFURIKO,KUOTA MAJI MENGI,KUOTA MAWIMBI.

KUOTA UNAOLEWA/UNAOA.

KUOTA UNAKOJOA KITANDANI.

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments