1.Naomba kuelezewa maana ya huu mstari tafadhali, unaosema; Mfalme wa Israel akajibu, akasema, Mwambieni ” Avaaye asijisifu kama avuaye ” huyu mfalme alikuwa anamaanisha nimi kusema hivyo? (1Wafalme 20:11)
JIBU: Hiyo ni mithali iliyokuwa inatumika wakati huo, kama leo watu wanavyosema “usitukane mamba kabla hujavuka mto”..Na hapo ni hivyo hivyo…hapo huyu Benhadadi alikuwa ameshajitangazia ushindi dhidi ya Israeli kabla hata ya vita…(Ni kama vile anameshawadharau anaokwenda kupigana nao kabla hata hajapigana nao), Ndio Mfalme Ahabu akamwambia avaaye asijisifu kama avuaye…maana yake avaaye mavazi ya vita ambaye ndio kwanza anakwenda vitani asijisifu kama yule mtu ambaye tayari ameshavimaliza vita na kashinda! na hivyo sasa anavua mavazi yake na kusherehekea ushindi..Hiyo ndio maana yake huo mstari.
Na ukifuatilia Habari hiyo utaona jinsi Mungu alivyowapigania Israeli kutokana na kiburi hicho cha mfalme wa Shamu, kuwadharau Israeli Pamoja na Mungu wao.
1Wafalme 20: 10 “Ndipo Ben-hadadi akatuma kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu.
11 Mfalme wa Israeli akajibu, akasema, Mwambieni, Avaaye asijisifu kama avuaye.
12 Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.
13 Na tazama, nabii akamjia Ahabu mfalme wa Israeli, akasema, Bwana asema hivi, Je! Umeona makutano haya yote walio wengi? Angalia, nitawatia leo mkononi mwako; nawe utajua ya kuwa ndimi Bwana”.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
NA MTU MMOJA AKAVUTA UPINDE KWA KUBAHATISHA, AKAMPIGA MFALME
About the author