Kwanini yule mtu afe kwa kuliwa na simba?

Kwanini yule mtu afe kwa kuliwa na simba?

Katika 1Wafalme 20:35-37, Kwanini yule mtu afe kwa kuliwa na simba baada ya kukataa kumpiga yule nabii?..je Mungu anaruhusu watu kupigana?

JIBU:Tusome

1Wafalme 20:35-37 “Basi, mtu mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake kwa neno la Bwana, Nipige, nakusihi. Akakataa yule kumpiga.

36 Akamwambia, Kwa sababu hukuisikiliza sauti ya Bwana, angalia, mara ukitoka kwangu simba atakuua. Na mara alipotoka kwake, simba alimwona, akamwua.

37 Ndipo akaona mtu mwingine, akasema, Nipige, nakusihi. Yule mtu akampiga, hata kumpiga na kumtia jeraha”

 Kuna wakati Mungu anatumia ishara za mwilini kuzungumza na watu wake au kufikisha ujumbe mahali..Kwamfano utaona Nabii Hosea aliambiwa aoe mwanamke wa kizinzi,

Hosea 1:2 “Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana”.

Lengo la Mungu kumwambia Hosea akaoe mwanamke wa kizinzi sio kuhalalisha uzinzi kwa watu wake, hapana bali ni kuwaonyesha watu wake jinsi na wao wanavyofanya uzinzi mbele zake kinyume chake katika roho…Hosea hakuwa mzinzi lakini aliambiwa akamwoe mwanamke mzinifu, ambaye ni kahaba mwenye wanaume wengi, ambaye hatulii. Sasa nafasi ya Hosea ambaye hakuwa mzinifu ilimwakilisha Mungu na huyo mwanamke wa kizinzi ililiwakilisha taifa la Israeli, kwa jinsi yule mwanamke alivyokuwa ni kahaba baada hata ya kuolewa na Hosea ndivyo Taifa la Israeli lilivyofanya uzinzi katika roho na kumwacha Mungu wao ambaye ndiye mume wao kama Isaya 55:5 inavyosema “Kwa sababu Muumba wako ni MUME WAKO; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote”

Sasa endapo Nabii Hosea angekataa maagizo yale Mungu aliyompa ya kwenda kumwoa mwanamke kahaba…na kusema hapana Bwana mimi sitaki kumuoa mwanamke yule ambaye ni mzinzi na kahaba hata nikimuoa bado ataendelea kuwapenda hao mabwana wake…Ni Dhahiri kuwa Hosea angetenda dhambi kwasababu amekataa shauri la Bwana la yeye kufanyika ishara kwa Israeli. Na hivyo angewafanya Israeli wasitubu, lakini ishara ile iliwafanya Israeli wengi watubu..Kwasababu walipokwenda kumuuliza wewe Nabii wa Mungu mbona unaoa mwanamke ambaye anamabwana wengi na zaidi ya yote tunamwona mkeo huyo yupo na mabwana wengine, unajisikiaje kwa hilo?..Ndipo Hosea atawajibu ni mfano wa nyinyi mlivyomwacha Mungu wenu ambaye ni mume wenu na kuigeukia miungu mingine kuiabudu..Hivyo mrudieni Mungu wenu ambaye ni Mume wenu kwasababu amewakasirikia sana.

Halikadhalika kuna wakati Mungu alimwambia nabii mwingine amwambie mwenzake kwamba ampige mpaka apate majeraha…ili kwa kupitia yale majeraha aonekane kama alikuwa katika vita vikali na aende kwa mfalme wa Israeli akiwa na yale majeraha…Ili mfalme adanganyike na kuamini kuwa ni kweli alikuwa kwenye mapambano kwasababu ana majeraha..na ndipo ampe fumbo ambalo litamtega…Na kweli mfalme alipomwona mtu anakuja mwenye majeraha akasema bila shaka mtu huyu atakuwa ametoka vitani kwa majeraha yale..na alipopewa lile fumbo na yule nabii kumbe lilikuwa linamhusu mfalme mwenyewe..kwasababu alimwacha huru Benhadadi ambaye alipaswa kumuua kabisa..

Hivyo akaambiwa sehemu yake ataichukua yeye. Unaweza kuisoma vizuri habari hiyo katika 1Wafalme 20:35-43.

Lakini yule mtu alikataa maagizo yale ya Mungu..ingawa aliambiwa ni maagizo kutoka kwa Mungu lakini akakataa kumpiga..hakujua kuwa kwa kukataa kule kungemfanya mfalme wa Israeli asiyaamini maneno yale ya Mungu…Na ikasababisha dhambi kwake, na ndio mbeleni akaenda kuliwa na simba..lakini yule mwingine hakulichukulia lile jambo la kumpiga nabii wa Mungu kwamba ni jambo la kumuumiza..bali aliona mbele kwamba kwa ishara ile ya majeraha ya yule nabii, mfalme ataamini ujumbe kutoka kwa yule nabii sawasawa na Neno la Mungu na hivyo atakuwa ameyatenda mapenzi ya Mungu Zaidi.

Hivyo ni jambo la kawaida kabisa Mungu kuzungumza kwa ishara za mwili, alifanya hivyo kwa Hosea, Kwa Ezekieli, na kwa manabii wengine wengi.

Bwana atubariki

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

YEZEBELI ALIKUWA NANI

Kuna haja gani ya kumwamini Yesu aliyezaliwa kama sisi?

MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments