Maana ya Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia”.(Warumi 9:13)

Maana ya Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia”.(Warumi 9:13)

SWALI: Je Mungu anawapenda watu wote?..Kama ndivyo kwanini alisema mahali Fulani kwamba anamchukia Esau. (Warumi 9:13)


JIBU: Tusome,

Warumi 9:13 “Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia”.

Chuki inayozungumziwa hapo sio chuki ya kinyongo, kama sisi wanadamu tulizonazo…Sisi wanadamu tukimchukia mtu “tunatamani hata Yule mtu afe au apate madhara Fulani mabaya”…Chuki ya namna hii ni mbaya sana na inatoka kwa Yule mwovu.

Lakini chuki inayozungumziwa hapo katika Warumi 9:23 ni chuki ya “kutopendezwa na mtu”…Mungu wetu anawapenda watu wote lakini hapendezwi na watu wote. Hivyo andiko hilo sio la kulitafsiri kibinadamu au kimitazamo yetu ya kibinadamu…Tukilitafsiri kwa njia hiyo basi tutashindwa kumwelewa Mungu vizuri.. “kila mahali utaona kama biblia inajichanganya”

Mstari mwingine tena ambao unazungumzia chuki ambayo usipotafsirika vizuri ni rahisi kupoteza maana kabisa ni huu..

Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,

26 Kama mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.

Umeona hapo?…haimaanishi kwamba tuwachukie wazazi wetu na ndugu zetu, tusiwapende kabisa, kiasi kwamba hata tuwafanya kuwa maadui zetu ndio iwe tiketi ya sisi kumfuata Yesu na kukubaliwa na yeye…Hiyo sio tafsiri yake…bali tafsiri ya chuki inayozungumziwa hapo ni kitendo cha kuyakataa mapenzi ya ndugu zetu yanayokinzana na mapenzi ya Mungu, na kuchagua kufuata mapenzi ya Mungu zaidi ya mapenzi yao.

Kwamfano Baba/mama/ndugu anakwambia twende kwa mganga…ilihali wewe ni mkristo na unajua hayo sio mapenzi ya Mungu, hapo huna budi kuyakataa maamuzi yao na kufuata mapenzi ya Mungu…sasa kile kitendo cha wewe kuyakataa matakwa yao na kufuata matakwa ya Mungu…Mbingu inatafsiri kama “umemchukia Baba yako/Ndugu yako na umempenda Mungu”. Ingawa wewe upendo wa ndugu zako upo pale pale, unawaombea, unawahurumia, unawaheshimu na kuwajali na kuwatunza.

Ndivyo hivyo hivyo kwa Esau, Mungu hakumchukia kwa chuki za kibinadamu, kwamba hataki kumwona mbele zake, kwamba ni adui yake, na hata hataki kumweka akilini mwake…hapana! bali alimaanisha “hakupendezwa naye kwa matendo yake kama alivyopendezwa na Yakobo”.

Hivyo na sisi hatuna budi kumpendeza Mungu kila siku katika maisha yetu…ili yasitupate kama yaliyompata Esau.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je! Hamna nyumba za kulia na KUNYWEA?.Mstari huu unahalalisha unywaji wa pombe?

WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.

JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?

MWISHO WA DUNIA UTAKUJAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments